Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Dkt Ibrahim Mwangalaba akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
****************************
Na Magrethy Katengu
Benki ya Maendeleo Plc imepata faida ya shilingi Bilioni 1.3122 mwaka 2022 ukilinganisha na faida ya shilingi milioni 587 mwaka 2021 ambapo ni sawa na ongezeko la zaidi ya mara mbili ya faida iliyopata iliyochangiwa na ikiwemo kutoa mikopo ya riba nafuu,kupata wanahisa wapya,ulipaji wa gharama mbalimbali kupitia benki hiyo .
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Dkt Ibrahim Mwangalaba wakati akitoa ripoti ya ufanisi na utendaji kazi wa Benki hiyo Kwa mwaka 2022 ambapo amesema benki hiyo imeweka historian yenye faida kwa Miaka 8 tangu kuanza kufanya kwake kazi mwaka 2015 .
Dkt Mwangalaba amesema kuwa faida hiyo imetokana na ukuaji wa jumla wa mapato kwa asilimia 22 mwaka hadi mwaka kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 12.8 hadi shilingi za kitanzania Bilioni 15.6 mwaka 2022.
"Tunafurahi kuripoti matikeo mengine ya kifedha ya Mwaka thabiti yayoongeza ufaulu ambao Maendeleo benki imefanya Kwa mwaka 2022 kwani mwaka huo ilisajili ukusji wa faida 184% na 163% mwaka kwa mwaka faida baada ya kodi pia kupata wanahisa 8%mapato ya kila hisa shilingi 50 za kitanzania huku faida ya benki kabla ya kodi kuongezeka hadi kuongezeka shilingi bilioni 2.02 kutoka shilingi milioni 710 kwa mwaka 2021,"amesema Dkt Mwangalaba
Amesema kuwa Mapato halisi yaliongezeka Kwa asilimia 31 kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 7.6 mwaka 2021 hadi shilingi za kitanzania Bilioni 9.9 mwaka 2022,pamoja na biashara ya mikopo kutokana na kuimarika Kwa hali ya uchumi na kuboresha ubora wa vitabu vya mkopo kutoka mikopo chechefu asilimia 13 mwaka 2021 hadi asilimia 5.2 mwaka wa 2022.
"Amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 11 kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 70 mwaka 2021 hadi shilingi za kitanzania 77 mwaka 2022 wakati mikopo na malipo ya awali kwa wateja yaliongezeka Kwa asilimia 5 kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 57 Hadi shilingi za kitanzania Bilioni 60 mwaka 2022" amesema Dkt Mwangalaba.
Hata hivyo Mkurugenzi Dkt Mwangalaba wa Benki ya Maendeleo Plc amesema mafanikio ya benki hiyo Kwa. mwaka 2022 ilisaidia Wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo Machinga zaidi ya 2500 Kwa kuwapatia Elimu kwanza ksha kuekopesha kupitia vikundi vyao benki ilitoa bilioni 3 hivyo na wao wamekuwa wakurejesha kwa uaminifu hivyo mwaka huu dirisha liko wazi la kukopa vigezo na masharti kuzingatiwa .
"Mwaka huu 2023 Benki ya Maendeleo imeamua kuweka lengo kubwa la kusaidia kuinua vipato vya Wafanyabiashara hivyo tunatarajia kuwafikia Wamachinga zaidi ya elfu tano,pamoja na makundi ya Wanawake na vijana kuwapatia Elimu ya biashara na kuwapatia mikopo yenye riba nafuu Kwa wale watakaohitaji karibuni sana"amesema Mkurugenzi
Pia Benki hiyo ina matarajioa makubwa mno kusogeza huduma karibu na wananchi nchi mzima hivyo inatarajia kufungua tawi jipya Mbagala Jijini Dar es salaam,kuanzisha huduma za mtandao( Internet Banking) na huduma ya ulipaji na upokeaji wa malipo ( Payment Collection System) itakayotumika Kwa ajili ya kulipa ada mashuleni pamoja na kulipa gharama za matibabu hospitalini.
"Mfumo huu unasaidia kulipa ada au malipo ya gharama za matibabu hospitalini,mfumo huu ukilipa tu taarifa zinafika sehemu husika hakuna haja ya kupeleka risiti ya malipo ,tunafanya hivi Ili kuwaondolea wazazi usumbufu wa kupeleka risiti shuleni au hospitalini" amesema Dkt Mwangalaba.
Aidha ametoa wito kwa wale wote wanaoendesha shughuli zao za kiuchumi kwa kukopa kuwa waaminifu kurejesha madeni yao kwa wakati kwani kufanya hivyo inawajengea sifa nzuri hata katika mabenki mengine kukopeshwa pale wanapokuwa na uhitaji wa kifedha
0 Comments