Ticker

6/recent/ticker-posts

WATU WATATU (3) WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 18 KUJERUHIWA.



************

Na Sheila Katikula ,Mwanza

Watu watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine 18 kujeruhiwa baada ya gari lenye namba za usajili T879 CHF aina ya Tata pitu lililokuwa limebeba matofali kufeli bleki katika eneo la nyakato Mkoani Mwanza.

Akithibitisha kutokea Kwa ajiri hiyo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa chanzo cha ajiri hiyo ni lori kufeli bleki na kusababisha magari manne kugongana.

Mutafungwa amesema kuwa magari hayo yaliyopata ajari yalikuwa yamesimama ili kusubiri mataa kuruhusu kuendelea na safari huku dereva aliyesababisha ajili hiyo ametoroka.

"Ajiri hiyo ilitokea majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la nyakato sokoni magari yakiwa yanakusubiri taa yaruhusu ndipo likatokea lori lililofeli bleki na kusababisha ajari hiyo" amesema Mutafungwa.

Ametaja aina ya magari yalipata ajari hiyo ni T594 aina ya Toyota IACT, T604 CJK Toyota hiace, T419 DVN.

Mutafungwa ameeleza kuwa majerehi wote 18 wamefikishwa hospitali kupewa matibabu huku 15 wakiruhusiwa kurudi nyumbani na wengine watatu (3) kuendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.

Mutafungwa amewataka madereva kuendelea kufata sheria za barabarani na kukagua magari mara kwa mara ili kuepuka ajari.

Post a Comment

0 Comments