Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI 1,073,941 KUANZA KIDATO CHA KWANZA KWA AWAMU MOJA,2023


*Madarasa 8000 ya Rais Samia Yakamilika kwa 95%

OR- TAMISEMI

Naibu KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Dr. Charles Msonde amesema wanafunzi 1,073,941 waliochaguliwa kidato cha kwanza 2023 wataanza shule kwa wakati mmoja.

Hatua hiyo inafanya kusiwepo na utaratibu wa chaguo la pili (second selection) kama ilivyozoelekea kutokana na kukamilika kwa madarasa 8,000.

Dr. Msonde ameyasema ameyasema Wilayani kongwa wakati wa zaiara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa.

Alisema hakutakuwa na changuo la pili kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2023 na kuwasihi wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti shuleni kwa wakati.

" Kwa mwaka huu hakutakuwa na second selection (chaguo la pili la wanafunzi) kwasababu fedha zilizotolewa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu zimetosha kuboresha miundombinu ya kuwachukua watoto wetu wote kwa intake(mkupuo) mmoja ."

Amesema tangu Rais aingie madarakani ameshatoa fedha zilizowezesha kujenga zaidi ya vyumba vya madarasa 20,000 ndani ya miaka miwili hatua ambayo imewaondolea adha watoto kwa kuanza masono kwa pamoja huku wazazi wakiwa hawajachangishwa kitu.

Katika kukabiliana na ongezeko la wanafunzi kwa mwaka huu ametoa Sh bilioni 160 zilizotumika kujenga madarasa 8,000.

Ujenzi wa madarasa hayo nchi nzima umekamilika kwa asilimia 95.6 na yaliyobakia wako kwenye hatua za ukamilishaji.

Post a Comment

0 Comments