*************
NA OR-TAMISEMI
KITUO cha Afya Kisorya kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara wamemaliza mwaka kwa kishindo baada ya kufanya upasuaji wa kwanza wa kutoa mtoto.
Mganga Mkuu wa wilaya, Dkt. Jamali Kibambe amesema, kituo hicho kuanza kutoa huduma hiyo kutafanya kuwa na vituo vya kutoa huduma vinne ambavyo vinatoa huduma za upasuaji.
"Upasuaji wa kutoa mtoto umefanyika kikamilifu baada ya kupokea vifaa vya upasuaji kutoka Serikali Kuu mnamo mwezi Novemba,2022,"amefafanua.
Amehitimisha kwa kuishukuru Serikali kwa kuendelea kuwezesha vituo vya kutolea huduma za Afya kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.
0 Comments