Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI CCM MKOA WA MWANZA WATAKIWA KUWATUMIKIA IPASAVYO WANANCHI

Mwenyekiti Mpya wa chama Cha Mapunduzi Mkoa Wa Mwanza Sixbert Reuben akizungumza na wananchi kwenye hafla fupi ya mapokezi yaliyofanyika mkoani Mwanza

Wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakimsikiliza Mwenyekiti Mpya Sixbert Reuben akizungumza kwenye hafla ya mapokezi iliyofanyima mkoani Mwanza.

Mbunge wa jimbo la Sumve wilayani Kwimba,Kasalali Emmanuel amesema atahakikisha anashirikiana na viongozi wote waliochaguliwa ili waweze kuwatumikia wananchi.

*********************


Na Sheila Katikula,Mwanza.

Mwenyekiti Mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mwanza Bw.Sixbert Reuben amewataka viongozi waliochaguliwa kuanzia ngazi ya Matawi, Mashina na kata kuhakikisha wanawatumikia wananchi na siyo kuleta mambo yasiyofaa kwenye jamii.


Hayo ameyatoa wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika Mkoani hapa na kueleza kuwa Kila kiongozi anapaswa kuwa nyenyekevu na kuwatumikia wananchi.


Reuben amesema kila kiongozi anawajibu wa kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kuepuka migogoro itakayopelekea kukiangusha chama hicho.


Aidha ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani nchi nyingi za Afrika na Ulaya zilikuwa zimekubwa na janga la Uviko 19 pamoja na vita ya Ukraine na Urusi hivyo kupelekea Nchi hizo kukubwa na mfumko wa bei na siyo Tanzania peke yake.


"Uzalishaji mwingi na usafirishaji unahusisha mafuta hivyo nchi nyingi zilikuwa na mfumko wa bei kutokana na vita kutoka nchi za wenzetu" emesema Reuben.


Amesema kuwa pamoja na misukosuko yote iliyotokea bado Tanzania imebaki salama na mpaka sasa hakuna miradi ambayo inalegalega na hakuna mradi unaosubili kupewa pesa yote inakwenda kama ilivyopangwa.


Hata hivyo ameyataka makundi ya machinga na Bodaboda kumpa muda ili aweze kukutana nao ili kuona namna ya kuweza kutatua changamoto zao zinazowakabili.


Naye Mnec wa Mkoa Wa Mwanza, Jamal Babu amesema ni vema kila kiongozi kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa kujituma.


"Viongozi hawa ni maandalizi ya mwaka 2024/25 tunataka tushinde nafasi zote kwanzia kwenye viongozi wa Serikali za mitaa,madiwani,Wabunge na Rais,amesema


Baadhi ya viongozi waliochaguliwa wamempongeza Mwenyekiti kwa ushindi mkubwa alioupata na kumuahidi watahakikisha wanampa ushirikiano ili waweze kukisongesha chama mbele kwa masilahi mapana ya nchi na chama.


"Tutahakikisha tunatoka ushirikiano Kwa Mwenyekiti wetu ili tuweze kusonga mbele Kwa kuleta Maendeleo ndani ya chama cheti" Walisema.

Post a Comment

0 Comments