Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Waziri Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 20,2022 katika Ofisi za RITA Jijini Dar es Salaam Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Waziri Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 20,2022 katika Ofisi za RITA Jijini Dar es Salaam
***************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Waziri Ndumbaro amesema baada ya kuiwakilisha nchi katika Mkutano uliohusisha Mawaziri wa Sheria wa nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Mjini Balaclava, nchini Mauritius Novemba 22 hadi 25, 2022 umeleta matokeo chanya kwa Taifa letu kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 20,2022 katika Ofisi za RITA Jijini Dar es Salaam ambapo amesema Mkutano huo ulilenga kuimarisha mashirikiano na uelewa wa pamoja kwa Mawaziri wa Sheria katika masuala ya Sheria na Utawala wa Sheria kwa maslahi ya pamoja ya wanachama.
"Mkutano huo ulijikita katika kukuza na kuongeza kasi ya ufikiwaji haki kama inavyoongozwa na Mpango Kazi wa Ufikiwaji wa Haki kwa Wote uliopitishwa na Wakuu wa Nchi Wanachama Jijini Kigali, Mwezi Juni mwaka 2022". Amesema Waziri Ndumbaro.
Aidha, amesema Mkutano huo ulilenga kuimarisha haki za binadamu katika nchi wanachama ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya utelekezaji wa malengo endelevu yaliyoainishwa katika Ajenda ya Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa.
"Mawaziri tulikuwa tunabadilishana uzoefu wa namna bora ya kubadili mifumo ya haki na kutatua changamoto zake kwa lengo la kuhakikisha maisha ya wananchi katika Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola yanaimarika na kuondoa vikwazo vyote vya uiukaji wa haki za binadamu". Ameeleza Waziri Ndumbaro
Hata hivyo amesema katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo, nchi wanachama zimekuabaliana kuwa na utaratibu wa kuwateua mahakimu na majaji kutoka nchi moja ya Jumuiya ya Madola kufanya kazi katika nchi nyingine ya Jumuiya hiyo.
"Lengo hapa ni kuhakikisha wananchi wananchi zenye changamoto ya ufikiaji wa haki, zinakuwa na mifumo ya kuifikia kwa wakati na kwa gharama nafuu. Kwa muktadha huo, Mawaziri walikubaliana kuandaliwa kwa Kanuni na Miongozo ya namna bora ya kutekeleza suala la ushirikiano katika sekta ya Mahakama. Kanuni hizo zinaandaliwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola kwa Kushirikiana na Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Madola na Chama cha Wanasheria wa Jumuiya ya Madola". Amesema
Ameeleza kuwa kwa ujumla Mkutano huu ulilenga kuimarisha ushirikiano baina ya Nchi wanachama kwa lengo la kufungua fursa za ajira kwa watanzania hususani katika kada za majaji na Mahakimu kwa kuwa nchi wanachama watakuwa wakibadilishana na majaji na makamimu miongoni mwao na wengine kupata nafasi ya kufanya kazi katika nchi nyingine.
0 Comments