Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) akitoa maelezo kuhusu majani ya malisho ya wanyama katika shamba la taasisi hiyo katika ziara ya siku moja ya kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya maendeleo ya ufugaji mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa (TALIRI) Zabron Nziku akitoa maelezo kwa wajumbe wawakilishi wa kamati katika ziara ya siku moja ya kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya maendeleo ya ufugaji mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya siku moja ya kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya maendeleo ya ufugaji mkoani Tanga.
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaame Khamis akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya siku moja ya kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya maendeleo ya ufugaji mkoani Tanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Yussuf Hassan Iddi akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya siku moja ya kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya maendeleo ya ufugaji mkoani Tanga.
*******************
Na Hamida Kamchalla, TANGA.
SERIKALI nchini pamojana serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia viongozi wao kutenga siku moja ndani ya mwaka iwe ya Kitaifa kuhamasisha wananchi kuhusu unywaji wa maziwa.
Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Yussuf Hassan Iddi jijini Tanga walipofanya ziara ya siku moja ya kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya maendeleo ya ufugaji.
Aidha ziara hiyo imeanza kutembelea katika Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), pamoja na kiwanda cha kusindika maziwa cha Tanga Fresh zilizopo jijini Tanga, ambapo Mwenyekiti huyo pia aliikumbusha jamii kupenda kunywa maziwa kwakuwa yana faida nyingi.
“Niwaombe viongozi wangu wa Kitaifa kwa pande zote mbili kama itawapendeza kutenga siku moja tu ndani ya siku 365 ambayoitakuwa maalumu kuifanya iwe siku ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa kwa wananchi” amesema.
Aidha Iddi amewasisitiza wafugaji na wadau wanaofanya biashara ya maziwa na kiwanda cha Tanga Fresh wasikate tamaa ya kupeleka bidhaa zao badala yake wafanye makubaliano na kupeleka kwa wingi ili uzalishaji uweze kuongezeka.
“Tumeafikiana kwamba soko la maziwa lipo kubwa, hivyo wafuge kisasa zaidi ili waweze kupata maziwa mengi, na kiwanda hiki kinahitaji maziwa ya kutosha, tumeona kwasasa maziwa siyo mengi na ndiomaana uzalishaji siyo mkubwa” amesema.
Naye Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis amesema mbali na ziara hiyo kuwafunza mambo mengi lakini pia wamefurahishwa na mapokezi waliyopata kutoka kwa viongozi wa Mkoa.
“Moja ya vitu tulivyojifunza katika ziara hii kwanza ni jinsi ya Taasisi za Utafiti zinavyofanya kazi zake katika kuongeza kiwango cha uzalishaji hii itamsaidia mkulima wa Tanzania kuweza kuzalisha kwa kiwango kikubwa cha ubora” amesema.
Pia amebainisha kwamba katika yale waliyojifunza yapo baadhi ambayo Zanzibar hakuna hivyo kuahidi kwenda kuyafanyia kazi liutendaji na kuboresha
“Viongozi wetu wa serikali zote mbili wanakaa na kutuelekeza tufanye kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu, na lengo ni kuona kuwa sekta tunazoziongoza zinaendelea kunufaisha wananchi katika kujiongezea kipato” amebainisha.
Kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba, mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa amesisitiza ufugaji wa kisasa ili kuweza kuleta tija katika uzalishaji badala ya kufuga kimazoea huku uzalishaji ukiwa mdogo.
"Kwahiyo niendelee kutoa rai kwa wafugaji, waache kufuga mifugo kizamani, utakuta mtu ana ng'ombe wengi ambao hawazalishi kwa tija kwa siku anapata maziwa lita moja au nusu, badala yake wafanye ufugaji wenye tija ili kujiongezea kipato" amesema.
"Na kupitia fursa hii ya kutembelea na wenzetu waheshimiwa wabunge wameliona kwetu nasi tumewataka waende wakatoe elimu kwa wafugaji katika maeneo yao mbalimbali kule Zanzibar" amesema.
0 Comments