**************************
Na Zena Mohamed,Dodoma.
MKURUGENZI wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),CP Salum Hamdun amesema Tanzania ni kati ya nchi sita duniani zilizotangazwa kupiga hatua katika masuala ya mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini.
Pia amesema Tanzania imepanda nafasi ya 87 kwa mapambano dhidi ya rushwa kati ya nchi 187 ambazo zimefanyiwa utafiti na mashirika mbalimbali.
Mkurugenzi huyo amesema hayo jijini hapa leo,Desemba 20,2022 katika Mkutano Mkuu wa Mwaka unaoenda sambamba na uzinduzi wa Programu ya TAKUKURU rafiki yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya rushwa.
CP Hamdun ametaja nchi nyingine zilizopiga hatua ni pamoja na Ethiopia,Sisheli,Angola,Rwanda na Senegal ambazo zimepiga hatua kutokana na utafiti uliofanywa na mashirika mbalimbali likiwemo la Transparent International.
"Mapambano dhidi ya rushwa ni ya kila mmoja hivyo kila mtu anapaswa kumuangalia mwenzake anayehusika na vitendo dhidi ya rushwa na kutoa taarifa ambazo zinaviashiria vya rushwa"amesema.
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo amezungumzia kuhusiana na uzinduzi wa program Rafiki ya kupambana na rushwa ambapo amesema itapelekwa kila mahali mpaka kwenye kata ili iwasaidie wananchi kujua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao.
Akizungumza Kabla ya kufungua Mkutano huo pamoja na Programu ya TAKUKURU rafiki Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kufanya vipimo vya rushwa kwa kila mkoa nakuitangaza na ile itakayoonekana ina kiwango kikubwa Cha rushwa ijitafakari,
Huku akitaja lengo la kujitathmini ni kupimana na kuona ni mkoa upi ambao unakiwango kikubwa cha rushwa na upi unakiwango kidogo cha rushwa kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia watendaji kujitadhimini katika maeneo yao
Amesema kuwa mapambano yao wanayapeleka katika kupambana na rushwa lakini haiwakatazi na haiwaondoi kwenye majukumu yao ya kila siku kwani majukumu waliyopewa ni ya kushughulika na kupambana na rushwa ujenzi wa maadili na stahiki kwa watumishi wa umma
"Nyie makanda wangu wa Mikoa mahali pa kuanza ni kwa huyo Katibu Tawala msaidizi anayeshughulikia Utawala na rasilimali watu akiweza huyo kufanya kazi zake vizuri mienendo na vitendo vya unadhulifu wa fedha za taifa hili letu kwenye Halmashauri zitapungua ama kuisha kabisaa kutqneni nao hawa,"amesema.
0 Comments