Ticker

6/recent/ticker-posts

SiMBA SC YAZIDI KUIPUMULIA YANGA KILELENI, YAICHAPA GEITA GOLD 5-0



NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba imefanikiwa kuondoka pointi tatu na kufanikisha kufunga mabao 5-0 dhidi ya timu ya Geita Gold, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Simba Sc katika mchezo huo aliweza kutawala mchezo kuanzia katikati ambako kulisaidia kuzalisha mabao hayo ya aina yake.

Simba Sc kwenye kipindi cha kwanza walicheza kwa kushambulia na kufanikiwa kupata mabao ya haraka kupitia kwa mshambuliaji wao John Bocco akifungwa kwa kichwa huku goli la pili likifungwa na Chama.

Katika kipindi cha pili Simba ilirudi ikiwa inahitaji mabao mengi kwani imekuwa ikishambulia kwa kasi ndipo ikafanikiwa kupata mabao mengine matatu kupitia kwa nyota wao Sakho aliyefunga mawili na goli la mwisho amefunga Kibu Dennis ambaye aliingia kipindi cha pili.

Post a Comment

0 Comments