Ticker

6/recent/ticker-posts

NIT KUTUMIA FURSA YA UJENZI WA RELI KWA KUANDAA MAFUNZO


******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHUO cha Taifa Usafirishaji (NIT) kimeandaa Kongamano la Tisa la kuwapongeza wahitimu wa Chuo hicho waliofanya vizuri katika masomo ya nadharia na vitendo katika chuo cha Taifa cha usafirishaji ili kuwapa motisha na wengine waweze kufanya vizuri katika vipindi tofauti.

Akizungumza katika Kongamanohilo leo Desemba 8,2022 Jijini Dar es Salaam, Naibu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Prosper Mgaya amesema NIT wanajitaidi kutoa wanafunzi wenye weledi kwenye njia tano za usafirishaji, ambapo mwaka huu mada yao kuu ipo kwenye usafiri wa reli na wamefanya hivyo kwa sababu za kuzingatia Serikali inavyowekeza fedha nyingi katika usafiri wa reli.

Amesema Chuo kipo mbioni kuanzisha kitengo cha mafunzo ya usafiri wa reli mkoani Tabora, ambacho kitafadhiliwa na Serikali na ndiyo maana chuo kinafanya ukaribu na shirika TRC kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa ajili ya kuanzisha hicho kituo,

"Nchi yetu imekaa kwenye eneo la kimkakati ambayo nchi ya Congo na Burundi zinategemea nchi yetu ndiyo maana reli zitajengwa hadi kwenye hizo nchi ili tuweze kusafirisha mizigo kuja Tanzania," Amesema

Kwa upande wake, Mkurugenzi Uthibiti wa Barabara kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Aridhini (Latra), Johansen Kahatano ameipongeza NIT kwa mageuzi ambayo wameyafanya kwa kupanua wigo wa mitaala na kufikia maeneo mengi ya usafirishaji ikiwemo, barabara, reli , anga, maji na bomba.

Amesema NIT wameongeza wahitimu wengi na tumeshuhudia wahitimu wakifanya vizuri katika maonyesho ambavyo wamekuwa wakifanya kwemye makongamano mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika nchini.

Post a Comment

0 Comments