Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii CPA Munguabela Kakulima Wakati akifungua Mdahalo wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru lililoandaliwa na Chuo Cha Taifa cha Utalii Dar es salaam.
Meneja Chuo cha Utalii Kampasi ya Arusha Dkt Maswet Masinda akiendesha Mdahalo wa Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru katika chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam
Washiriki ya pamoja na Mgeni Rasmi waliohudhuria Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru
************************
Na Magrethy Katengu
Katika kuadhimisha Miaka 61 ya Uhuru Desemba 9 kila mwaka,Chuo Cha Taifa Cha Utalii kimesema kitaendelea kuweka jitihada ya kutoa Mafunzo bora ya ukarimu(Hospitality) kwa wanafunzi yatakayokuwa chachu ya kuongeza idadi ya Watalii nakufikia lengo la Watalii milioni tano ifikapo 2025.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii CPA Munguabela Kakulima katika Mdahalo wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika lililoandaliwa na Chuo hicho kwa lengo la kujadili mafanikio ya sekta ya Utalii Kwa miaka 61 iliyopita na nini kifanyike katika miaka ijayo Ili kukuza Utalii ndani na nje ya nchi
Hata hivyo CPA Munguabela amesisitiza kuwa chuo cha Taifa cha Utalii kimekua kikiwajengea uwezo wahudumu wanaofanya kazi za kupokea Watalii wa ndani na nje ya nchi kwani wao ndio kundi pekee la linalokua karibu na Watalii kuanzia muda wanapoingi Hadi wanapoondoka katika maeneo wanayofikia ikiwemo hotelini na Hifadhi mbalimbali za Utalii.
" Tunaelekea kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru tunajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kipindi tunapata Uhuru hadi sasa ikiwemo idadi ya Watalii kutoka nje ya nchi kuongezeka ,lakini pia tumejua Utalii vyuo vyetu vya Utalii lazima wanapatiwa Mafunzo ya ukarimu wafundishwe mbinu nyingi za kuutangaza utalii uliopo kwani wao ndio hujua nini,na mtalii anahitaji nini kwakweli kuna Mabadiliko makubwa "amesema Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii.
Kwa upande wake Meneja Chuo cha Utalii Kampasi ya Arusha Dkt Maswet Masinda amesema Sasa Dunia inakwenda na Sayansi na Teknolojia hivyo namna Utalii tunavyouendesha Sasa ni tofauti na miaka ya nyuma hivyo kupitia Vyuo vyote vya Utalii havina budi kuwapa Mafunzo wanafunzi Kwa kutumia Teknolojia ili hata watalii wanapowakarimu watamani kurudi tenaa.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Ernest Mwamwaja amesema kwamba sekta ya Utalii kwa Sasa imekuwa sana kwani katika kipindi hiki imekua ikiendeshwa kidigitali tofauti na miaka ya nyuma ambapo matangazo mengi ya Utalii yanafanyika mtandaoni na Rais Samia Suluhu Hassani aliiongeza bajeti ya kutosha Bodi ya Utalii ili ijitanganze kupitia mitandao .
Mwamwaja amesema kwamba hapo nyuma serikali pekee ndio ilikua inaendesha sekta ya Utalii hivyo kwa sasa kuna hatua kubwa kwani makampuni mengi ikiwemo ya ndani na nje ya nchi yameruhusiwa kuwekeza katika sekta ya Utalii ikiwemo kujenga hoteli,kumiliki vitalu vya Utalii,kujenga vyuo vya Mafunzo ya Sekta ya Utalii.
"Hadi kufikia 2025 serikali imepanga kupata idadi ya Watalii milioni 5, na kupata fedha za kigeni dola Milioni 7, kwa Sasa Watalii wamefikia milioni 1.5, hali hiyo pia imechangiwa na Rais Dr.Samia Suluhu Hassani kupitia filamu ya Tanzania the Royal Tour ambayo imeitangaza Tanzania kidunia na Watalii wanazidi kumiminika hapa nchini" amesema Mwamwaja.
Kongamano hilo limewakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo Wanazuoni,Wasomi,Wanafunzi lengo ni kujadili hali ya Sekta ya Utalii kuanzia kipindi kilichopita na kilichopo kwa sasa nakuweka maazimio ya nini kifanyike ili kufikia malengo ya 2025 yakuongeza Watalii zaidi.
0 Comments