Ticker

6/recent/ticker-posts

LICHA YA CHANGAMOTO YA USAFIRI ZAHANATI YA BAGA ILIYOPO MOROGORO VIJINI MSD YAENDELEA KUPELEKA HUDUMA


Matukio mbalimbali katika picha ambazo zinaonesha namna Bohari ya Dawa inapeleka dawa na vifaa tiba kwenye Zahanati ya Baga iliyopo Morogoro vijijini.Changamoto kubwa ni usafirishaji dawa kutokana na zahanati hiyo kuwepo kwenye miiinuka mikubwa inayotokana na safi ya Milima Uruguru

************************

Na Mwandishi Wetu

CHANGAMOTO ya miundombinu ya usafirishaji katika baadhi ya maeneo pamoja jeografia ya nchi yetu inailazimu Bohari ya Dawa (MSD) kutumia gharama za ziada katika kuhakikisha huduma ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi inafika kwa wananchi.

Zahanati ya Baga iliyopo Mnewele mkoani Morogoro ni kielelezo cha maeneo yaliyogubikwa na changamoto hizo kutokana na jiografia ya eneo hilo ambalo liko kwenye safu ya Milima Uruguru ambapo ili kufika inahitaji kupita kwenye barabara zilizopo milimani.

Hivyo ni vigumu kutumia usafiri wa gari moja moja hali inayowalazimu MSD kutumia gharama za ziada kwa ajili ya kukodisha pikipiki na baadaye watu kwa ajili ya kubeba kichwani ili kuhakikisha ili dawa na vifaatiba zinafika kwenye Zahanati ya Baga ambayo pia inalazimu anayesafirisha dawa au vifaa tiba kuvuka mito miliwi mikubwa.

Pamoja na mazingira magumu ya kufikisha dawa na vifaa tiba kwenye zahanati hiyo ya Baga ambayo pia inaakisi mazingira ya jiografia ya maeneo mengine yenye milima , mito na mabonde MSD imeendelea kusisitiza itaendelea kupeleka huduma hiyo muhimu kwa wananchi bila kujali ugumu wa kuifikisha , lengo ni kuona wananchi wanapata dawa na vifaa tiba jirani huduma za afya zilipo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Maofisa wa Bohari kutoka Kanda ya Dar es Salaam waliotembelea Zahanati ya Baga mkoani Morogoro, Mfamasia wa MSD Kanda ya Dar es Salaam Diana Kimario amesema kuwa iwe jua , iwe mvua wao wataendelea kupeleka na kufikisha huduma ya dawa na vifaa tiba.

Ameongeza wanatambua mazingira yenye ugumu kufikika lakini MSD imejipanga vema kuhakikisha huduma zinafika, akitolea mfano wa Zahanati ya Baga ambayo pamoja na changamoto ya kufikika kwa urahisi lakini bado wameendelea kuhudumiwa nyakati zote.

Kwa upande wake dereva wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Said Tindwa amesema kwa hali ilivyo ni vigumu kufika na gari."Gari unaenda nayo kama kilometa tatu kutokea barabara kuu, unafika eneo linaitwa Mtombozi hapo ndipo gari inaishia, hadi kufika ilipo zahanati ni safari ya takriban kilometa 60.”

Katika safari hiyo, alieleza baadhi ya maeneo yanapitika kwa bodaboda na mengine wanalazimika kukodi watu wabebe mzigo kichwani hadi ilipo zahanati ya Baga."Safari ya pikipiki ni kama nusu saa inakufikisha mtoni hapo pikipiki haiwezi kwenda tena tunawalipa watu wabebe mzigo kwa kichwa safari ya masaa mawili hadi wanafika.

Wajati wa ziara hiyo waandishi wa habari na maofisa wa MSD walilazamika kukodisha pikipiki ambapo kila kipikipi gharama ya nauli ilikuwa Sh.18,000 na hiyo ni kufika tu eneo la mto bila kuvuka mto na kuanza safari ya Baga ambayo iinakuzalimu kutumia saa mbili hadi tatu kwa kutembea kwa miguu ili kufika.

Pamoja na hayo yote MSD katika jukumu lake la kusambaza dawa kwa wateja kiutaratibu hufikisha dawa hizo moja kwa moja hadi kituo husika na kufanya makabidhiano mbele ya Kamati ya afya ya eneo husika.

Muuguzi Mkuu wa Zahanati ya Baga Sara Manyagi ameishukuru MSD kwa kuhakikisha bidhaa za afya wanazoomba zinapatikana za kutosha na kwa wakati pamoja na changamoto za kijiografia.

“Tunayafahamu mazingira yetu ni magumu sana kufikika lakini tunaishukuru MSD imekuwa ikituhudumia na jambo nzuri zaidi wamekuwa wakigharamia gharama zote za usafiri , hili kwetu linatufanya tuone MSD ni mkombozi wetu maana ili tutoe huduma bora lazima tuwe na dawa na vifaa tiba na kwetu vinatufikia kadri tunapohitaji,”amesema Mangagi.

Post a Comment

0 Comments