Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akizungumza kwenye Jukwaa la vijana Balehe kuadhimisha ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
SHIRIKA la Fikra Mpya limeendesha Jukwaa la vijana rika balehe mkoani Shinyanga (Youth Cafe), ambao wapo ndani na nje ya shule, na kuwapatia elimu mbalimbali juu ya mustakabali wa maisha yao na kuzifikia ndoto zao.
Jukwaa hilo limefanyika leo Desemba 9, 2022 katika ukumbi wa Katemi Hoteli Mjini Shinyanga na kukutanisha vijana mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akizungumza kwenye Jukwaa la vijana balehe, amesema katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, wameendesha Jukwaa hilo ili kutoa elimu ya ukatili kwa vijana pamoja na kuwapatia elimu ya kujitambua, maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, afya ya uzazi, na matumizi sahihi ya mitandao.
Amesema vijana ni nguvu kazi ya taifa, hivyo wanapaswa kupewa elimu mbalimbali ambao zitawaongoza katika maisha yao na kuzifikia ndoto zao, na hatimaye kuja kuwa tegemeo la taifa na viongozi mbalimbali.
“Shirika la Fikra mpya tunaamini maarifa pekee na elimu ya kujitambua ndiyo chanzo cha mafanikio kwa kila kijana na kuzifikia ndoto zake, ndiyo maana tukaanzisha jukwaa la vijana balehe, kuanzia umri wa miaka 14 hadi 25 walio ndani na nje ya shule na kuwapatia elimu ya makuzi,”amesema Josiah.
“Kiu yetu kubwa kama Fikra Mpya ni kuwafikia vijana wengi walio ndani na nje ya shule, sababu uhitaji wa elimu kwa vijana ni mkubwa ili kuzifikia ndoto zao, na kundi la vijana ni tunu kwa taifa, lakini tunashindwa kuwafikia kwa wingi sababu ya ukosefu wa Rasilimali fedha, tunaiomba Serikali pamoja na wadau mtushike mkono,”ameongeza.
Nao baadhi ya wazazi ambao wamehudhuria Jukwaa hilo akiwamo Paulina Sayi, wamewataka vijana mafundisho ambayo wamepatiwa wayazingatie kwa ajili ya manufaa ya maisha yao.
Naye Katibu wa kamati za ulinzi wa wanawake na watoto (Mtakuwwa) mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, amewataka vijana wajitambue pamoja na kuacha kujiingiza katika mambo yasiyofaa ambayo yataharibu ndoto zao, huku akiwataka pia wanapofanyiwa vitendo vya ukatili au kuona mtoto akifanyiwa ukatili watoe taarifa.
Nao baadhi ya vijana hao akiwamo Veronica James, wamesema mafunzo waliyoyapata kwenye Jukwaa hilo, yamewasaidia kujitambua na watayazingatia ili kuzifikia ndoto zao.
Aidha, Kauli mbiu ya Jukwaa hilo la vijana Balehe (Youth Cafe 2022) inasema KIJANA WAJIBIKA, KOMESHA UKATILI.

Katibu wa Kamati za ulinzi wa wanawake na watoto (Mtakuuwa) mkoani Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye Jukwaa hilo la vijana Balehe.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Afrika Intiatives Jonathan Manyama akizungumza kwenye Jukwaa hilo la Vijana Balehe.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake Laki Moja Mkoa wa Shinyanga Anascholastika Ndagiwe akizungumza kwenye Jukwaa hilo la Vijana Balehe.
Mzazi Paulina Sayi akizungumza kwenye Jukwaa hilo la vijana Balehe.
Waongoza mada wakiwa kwenye Jukwaa hilo la vijana Balehe.
Jukwaa la vijana Balehe likiendelea.
Jukwaa la vijana Balehe likiendelea.
Jukwaa la vijana Balehe likiendelea.
Peter Amani kutoka Shirika la Agape akiongoza majadiliano kwenye Jukwaa la Vijana Balehe.
Jukwaa la vijana Balehe likiendelea.
Picha za Pamoja zikipigwa mara baada ya kumalizika kwa Jukwaa hilo la Vijana Balehe.

0 Comments