Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR), Bi. Mahoua Parums, aliyemtembelea na kufanya naye mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR), Bi. Mahoua Parums, aliyemtembelea na kufanya naye mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR), Bi. Mahoua B. Parums, ambaye alimtembelea na kufanya naye mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR), Bi. Mahoua B. Parums, akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), alipomtembelea katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam ambapo walijadili masuala ya kuhudumia wakimbizi waliopo nchini.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimsindikiza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) Bi. Mahoua B. Parums baada ya kumaliza mazungumzo yao yalichofanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
(Picha na WFM – Dar es Salaam)
*********************
Na Benny Mwaipaja, DSM
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limeipongeza Tanzania kwa kuhifadhi wakimbizi wanaokimbia nchi zao kutokana na machafuko ya kisiasa na vita vinavyojitokeza katika mataifa yao.
Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo Bi. Mahoua Parums, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Bi. Mahoua amemweleza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Tanzania ni mfano wa kuigwa na mataifa mengine kutokana na sera zake nuri za kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi katika ardhi yake.
Alisema hadi sasa Tanzania imewapokea wakimbizi zaidi ya 162,000 kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo wanaotoka katika nchi za Burundi na Somalia ambao wameanza kurejeshwa makao baada ya hali za kisiasa kutengemaa katika mataifa yao.
Aidha, Bi. Mahoua Parums alisifu hali ya utulivu wa kisiasa Pamoja na hali ya amani na upendo wa Tanzania, hali inayovutia idadi kubwa ya wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alimweleza Kiongozi huyo wa Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Bi. Mahoua Parums kuwa Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuendeleza utulivu wa kisiasa ili kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi.
Alisema kuwa Tanzania inaendelea kusimamia vizuri uchumi wake licha ya changamoto mbalimbali ikiwemo athari zinazotokana na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine.
Alisema kuwa uchumi wa nchi umeendelea kukua kwa wastani wa asilimia 4.7 na baada ya miaka mitatu ijayo, uchumi unatarajiwa kuimarika na kukua kwa wastani wa asilimia 6 hadi 7.
Alimweleza Kiongozi huyo kuwa jitihada kubwa zinazowekwa na Serikali za kuimarisha sekta zinazochochea ukuaji wa haraka wa uchumi zikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi, zitachochea ukuaji wa ajira kwa makundi ya vijana na hatimaye kuchangia ukuaji wa pato na uchumi wa taifa.
Wawili hao, wamejadili kwa kina kuhusu hali ya wakimbizi waliopo nchini na namna ya kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi na wakimbizi wanavyoweza kusaidiwa kwa njia ya kuwapelekea miradi mbalimbali ya kijamii kama shukrani kwa ajili ya kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi katika maeneo yao.
0 Comments