Ticker

6/recent/ticker-posts

ARGENTINA MABINGWA KOMBE LA DUNIA 2022


NA EMMANUEL MBATILO


TIMU ya Taifa ya Argentina imeibuka mabingwa kombe la Dunia kwa mikwaju ya Penati dhidi ya timu ya Taifa ya Ufaransa mara baada ya kutoka sare ya 2-2 kwa dakika 90 na 3-3 dakika 30 za nyongeza (extra time).

Argentina ilianza kutangulia kwa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa kipindi cha kwanza kupita kwa nyota wao Lionel Messi pamoja na Angle Di Maria na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele.

Kipindi cha pili Ufaransa ilifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji wake, mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwani walipata mabao mawili ya haraka kupitia kwa kijana wao nyota Kylian Mbappe na kumfanya amzidi mpinzani wake Lionel Messi kufikia mabao saba wakati mweznake akiwa na mabao sita tu kwenye michuano hiyo..

Post a Comment

0 Comments