Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) Dkt. Mboni Ruzegea akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam
*************
Na Magrethy Katengu
Bodi ya huduma za maktaba Tanzania(TLSB) imetoa wito kwa waandishi na wachapishaji wa majarida na vitabu kufuata sheria na taratibu zilizowekea ikiwemo kupelekea kopi mbili za machapisho yao pamoja na kazi ya kidijitali katika maktaba hizo ili kuweka kumbukumbu itakayosaidia kizazi kijacho kupata maarifa .
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) Dkt. Mboni Ruzegea amesema huduma za maktaba, utunzaji nyaraka na kutoa mafunzo ya ukutubi katika uboreshaji wa elimu Tanzania ..
Hata hivyo amesema Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la pili la kitaifa la huduma za maktaba linalotarajiwa kufanyika Novemba 23 hadi 24 mwaka huu Jijini Tanga likikutanisha wadau kutoka sehemu mbalimbali ili kujenga Taifa lenye kupenda kusoma ambapo mada kuu ya kongamano hilo ni mchango wa huduma za maktaba, utunzaji nyaraka na mafunzo ya ukutubi katika uboreshaji wa elimu Tanzania.
Sanjari na hayo amesema lengo kuu la kongamano hilo ni kutoa fursa kwa wadau wote wa huduma za maktaba nchini kushiriki kuchangia na kuamua kwa pamoja namna bora ya kuendesha huduma za maktaba nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.
"Niseme kuwa tumekuwa na Maktaba za ndani ya Mikoa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijulikana lakini madhari zake siyo nzuri kuvutia Waandishi na wasomaji kuzitumia hivyo kupitia kongamano hili tutakuja na nini kifanyike kuziboresha "amesema Dkt Mboni
Hata hivyo ametoa wito kwa waandishi na wachapishaji wa majarida na vitabu kufuata sheria na taratibu zinazotakiwa za kupelekea kopi mbili za machapisho yao pamoja na kazi ya kidijitali katika maktaba hizo ili kuweka kumbukumbu na kuwawezesha watu wengine kupata vitabu hivyo na kuvisoma.
0 Comments