Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WA HANDENI WAANZA KUNUFAIKA BOMBA LA MAFUTA, VISIMA VYA MAJI VYACHIMBWA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akimsikiliaza DC Mchembe akimfafanulia jambo wakati wa kikao na wadau wa Kampuni ya inayotekeleza ujenzi wa kambi namba 15 ya ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda.
Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa Ccm Wilaya ya Handeni wakifuatilia kikao hicho.


*********************

Na Hamida Kamchalla, HANDENI.


UJENZI wa mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda kuja nchini umeanza kuleta matunda kwa wananchi wa kata za Misima na Mabanda ambao wameanza kuondokana na kero sugu ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama wilayani Handeni.

Katika Wilaya hiyo ujenzi huo ambao unaotekelezwa ujenzi wa kambi namba 15 umepita katika eneo la Mabanda ambako licha ya wananchi waliopitiwa kulipwa fidia zao pia wameweza kunufaika na huduma maji baada ya Kampuni inayotekeleza mradi huo kuchimba visima viwili ambavyo vinatoa maji ya kutosha.

Akitoa taarifa ya utekelezaji Meneja wa mradi huo wa kampuni ya JV SPEK Mhandisi Alnord Siliro amesema kazi ya ujenzi wa mradi wa kambi hiyo umegharimu shilingi bilioni 8.9 amba ulianza august 12 na wanatarajia kukamilisha mradi desemba 24 mwaka huu huku utekelezaji wake mpaka sasa umefikia zaidi ya asilimia 46.



"Tulifanya taratibu zote za matakwa na kupata vibali mapema ili tusipate matatizo baadae na tufanye kazi kwa muda, na mpaka sasa sisi JV SPEK tuko kwenye asilimia 46.8 ya utekelezaji wetu na ikifika desema 24 kazi yetu tutakuwa tumemaliza" amesema.


Amesema walipofika eneo hilo hapakuwa na maji ya kutosha hivyo kuamua kuchimba kisima ambacho awali hakuweza kutoa majibya kutosha kufanya utekelezaji ndipo wakachimba kingine ambacho sasa kinatoa maji yanayowatosheleza na mengine kuwasaidia wananchi wa jirani na eneo hilo.


Aidha amebainisha kwamba katika utekelezaji wao wamefanikiwa kufuata matakwa ya mkataba walioingia na serikali kwa kuanza kulipa fidia wananchi wote ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi lakini pia wanawalipia pango ndani ya miaka mitatu huku wakiendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwemo maji.


"Tutakapokuwa tumemaliza utekelezaji wa mradi wetu na kuondoka, basi visima hivi tutawaachia wananchi wa Mabanda na watu wa Handeni kwani haya maji yaliyokuwepo hapa yanaweza kutosheleza watu wengi" amebainisha.


Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Handeni Mwajuma Ukwaju amesema mradi huo umekuwa chachu kwa Wilaya ya Handeni kwani mji umekua kibiashara na kuchangia kuongeza mapato kwakuwa Kampuni hiyo inafuata matakwa ya mkataba kwa kununua vifaa vya ujenzi ndani ya Wilaya hiyo.


"Niseme tu mradi huu kuletwa hapa kwetu na kuamua kujenga hapa Mabanda unetunifaisha kwa kiasi kikubwa kutokana na kutulete ajira kwa vijana wetu lakini pia mapato yetu ya halmashauri yameongezeka na kufanya uchumi wa Handeni kukua,


Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema mradi huo siyo tu utafungua fursa za Wilaya ya Handeni bali pia Mkoa kwa ujumla kwani umepita katika Wilaya sita za Handeni, Kilindi, Muheza, Korogwe, Tanga, na Mkinga.


Aidha ameishukuru kampuni hiyo kwa kuelezwa mkataba wao wa kutumia watu na vitu ndani ya Wilaya husika kwa kutoa ajira kwa vijana huku akiwasisitiza kuendelea kuzingatia mkataba huo kwa kufanya kazi nzuri itakayo wawezeaha kuonekana na kupewa kazi nyingine inapotokea uhitaji.


"Ninawashikutu sana na niwapongeze sana Kampuni ya kwa kazi nzuri mnayofanya, lakini pia mmejitoa kwa kiasi kikubwa, ujenzi huu kufikia asilimia 48 kwa muda huu ni kazi kubwa mmefanya, na kutuhakikishia kwamba ifikapo disemba 24 mwaka huu mradi utakuwa umekwisha, hongereni sana" amesema.


"Wito wangu kwenu, mzingatie matakwa ya mkataba, mradi huu ukamilike kwa wakati ili mjitengenezee jina zuri muweze kupewa kazi nyingi zaidi na serikali pamoja na hawa wadau wenu waliomipa kazi hii,


"Lakini jambo la faraja ambalo mnatuachia hapa Mabanda tunafaifika moja kwa moja na mradi huu, pamoja na manufaa mengine ya ajira, mapato kuongezeka na Uchumi kujua, hili suala la maji ni kubwa zaidi, kero ya maji ya miaka mingi sasa imekwenda kutatuliwa ndani ya miezi sita, tunaishukuru sana" ameongeza Mgumba.

Post a Comment

0 Comments