Na Shemsa Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewaapisha wajumbe wanne wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kyerwa na kuwataka watende haki, wafanye kazi kwa weledi na kuhakikisha wanatatua migogoro ya wananchi kwa kufuata sheria .
Akizungumza na wajumbe hao mara baada ya kuwaapisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Albert Chalamila amewataka wajumbe hawa kufanya kazi kwa uaminifu, kupunguza mashauri na kuepeuka kupokea rushwa kwani rushwa inakandamiza haki ya wanyonge
“Rushwa ni adui mkubwa wa mabaraza ya ardhi,wengi mnaapa halafu mnakwenda kukengeuka, kuwanyanyasa na kuwaonea watu mwisho tuhuma zinarudi baraza la ardhi mnanyanyasa watu.Sasa mkashughulikie mashauri na kutenda haki,”ameeleza Mhe. Chalamila
Sambamba na hayo amewataka kupunguza mirorongo mrefu wa kushughulikia mashauri hasa ya mirathi kwa upande wa nyumba na ardhi,wengi wamekuwa wanafoji nyaraka hali ambayo imepelekea migogoro na kushauri kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa watu mbalimbali ili kuwezesha kupunguza migogoro hiyo
Amewasisitiza kuepuka kufanya kazi kwa maelekezo kufuata sheria zinazowaelekeza katika kutafuta mashauri na kufanya kazi kwa weledi walioapishwa ni Elias Tigelindwa,Ezra Rugakira, Estha Mutafuta na Joileth Godwin .
Wajumbe hao uteuliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba, Makazi na Maendeleo ya Watu baada ya kushauriana na Mkuu wa Mkoa husika kwa mujibu wa kifungu cha 26 (1) cha sheria ya Mahakama za utatuzi wa migogoro ya Ardhi Sura 216 (2019).
Wajumbe hao watatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mihula miwili. Na majukumu yao ni kutoa ushauri kabla ya Mwenyekiti hajatoa uamuzi.
0 Comments