Ticker

6/recent/ticker-posts

TRC YAINGIA MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA SSRST UNUNUZI WA MASHINE NA MITAMBO 26 YENYE THAMANI YA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 51

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa(kulia) akibadilishana mkataba na ,Makamu wa Rais wa Kampuni ya SSRST kutoka Korea Kusini K.Charles Park baada ya kusaini mkataba wa ununuzi wa mashine na mitambo tofauti tofauti 26 kwa ajili ya matengenezo ya njia ya SGR, hafla ambayo imefanyika leo Novemba 7,2022 Jijini Dar es Salaam.


*****************


Na Magrethy Katengu.


Shirika la Reli Tanzania limeingia makubaliano ya ununuzi wa mashine na mitambo tofauti tofauti 26 kwa ajili ya matengenezo ya njia ya SGR kati ya TRC na Kampuni Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRSY) kutoka Korea Kusini yenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani Millioni 51


Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji Saini Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema lengo la ununuzi wa mashine na mitambo ni kuongeza ufanisi wa matengenezo ya njia na kupunguza matengenezo ya njia ya watu pia mitambo hiyo itaipa uwezo TRC kutunza mradi huo wa SGR muda wote wa uendeshaji


"Tutajipanga vizuri katika kuhakikisha usalama wa uendeshaji Treni hiyo ya Umeme kwani miongoni mwa mitambo na mashine pamoja na Fire fighting Road-Reli Vehicle (Mtambo wa kuzima moto sehemu mbalimbali za reli ikiwemo katika mahandaki kama ikitokea hitilafu ya umeme )na Overhead caternal system inspection car (Gari la kukagua miundombinu ya umeme" amesema Kadogosa.
.
Hata hivyo Mkurugenzi Kadogosa alibainisha vifaa hivyo Mobile flash butt Welding plant( Mtambo wa kuunganisha Reli Kwa welding),Track Inspection (Mashine ya Ukaguzi wa njia )Ultrasound vehicle (Mashine ya Ukaguzi wa njia),Weed Killing Trac Motorcar(Mtambo wa kuua majani yanayoota pembeni ya reli.


Naye Mwenyekiti wa bodi Wakurugenzi Shirika la reli Tanzania Prof John Kondoro alisema TRC imekuwa na Mabadiliko makubwa katika uendeshaji wake kwani miaka ya huko nyuma bendera zilikiwa zikitumika kutoa taarifa kuwa ni wakati abiria wa kupanda hivyo Kwa Sasa iko tofauti.


"Niishikuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe rais Samia Suluhu Hassani kwa juhudi zake anazozifanya miradi mikubwa kama SGR inajengwa Kwa kutumia gharama kubwa na Watumishi wako wanaendelea kupatiwa Mafunzo namna uendeshaji Mitambo na Mashine"amesema Prof Kondoro.


Naye Makamu wa rais wa Kampuni SSRST kutoka Korea Kusini K.Charles Park na Balozi wa Korea Kusini Kim Sun Pyo walisema Nchi yao uchumi wa Reli na Treni ndiyo uti wa mgongo wa Taifa lao hivyo kupitia mashirikiano hayo Tanzania wataisaidia iendelee kusonga mbele na kupiga hatua.


Post a Comment

0 Comments