Kikosi cha timu ya TRA SC kilichocheza NSSF na kuwabamiza mabao 2-0,mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga.
Na Oscar Assenga,TANGA.
MABINGWA Watetezi wa Michuano ya Shimuta kwa upande wa mpira wa Miguu Mfululizo TRA Sports leo imefanikiwa kutinga katika Hatua ya 16 bora katika Mashindano hayo baada ya kuibamiza timu ya NSSF mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga.
Katika mchezo huo ambao ulianza kwa kasi huku kila timu ikitaka kuondoka na alama tatu ili kuweza kujiweka kwenye mazingira mazuri,TRA SC ambao walikuwa na wachezaji mahiri wa mpira wa miguu waliweza kuusoma mchezo huo mapema na hivyo ikawa rahisi kwao kuutawala.
Wakionekana kucheza kwa kusikilizana huku wakipiga pasi fupi fupi na ndefu TRA SC waliweza kufanikiwa kufanya mashambulizi mfululizo mara kwa mara langoni mwa wapinzani wai na kuweza kuandika mabao yao kupitia Benzema na Max ambayo yalitosha kuipelekea timu hiyo hatua ya 16 bora.
Baada ya kumalizika kwa ,mchezo huo, Meneja wa Timu hiyo Gasaya Sereria amesema ni maandalizi mazuri ndio yaliyoifanya timu yao ishinde katika mchezo huo muhimu uliowahakikishia kuongoza kundi lao.
Gasaya amesema mchezo huu ulikua ni muhimu kwao kushinda kwa kua ulikua unawahakikishia kuingia hatua ya 16 bora.
Alisema kwamba wao kama mabingwa watetezi wamedhamiria kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi kwenye michezo yao ili kuweza kunyakua ubingwa huo kwa mara nyengine.
"Kwa kua sisi ni mabingwa watetezi mara mbili mfululizo,kusudio letu kubwa ni kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo,ndio lengo letu kuu katika mashindano haya"alisema Gasaya
Awali akizungumza mara nahodha wa TRA Sports,Mohamed Ayubu amesema mchezo huu ulikua inaamua hatma ya timu itakayoshinda ndio itakayoingia hatua ya 16 bora.
Hata hivyo alisema kwamba wao lengo lao kama timu pamoja na uongozi ni kuhakikisha tunachukua kombe hili kwa mara ya tatu,kwa sababu wana uwewzo wa kufanya hivyo kutokana na uimara wa kikosi walichonacho
0 Comments