Kikosi cha timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanawake
Na Oscar Assenga, TANGA
TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya kuvuta kamba kwa upande wa wanaume leo wameibuka kidedea kwenye mchezo wa kuvuta kamba baada ya kuwavuta timu ya Benjamini Mkapa Hospitali kwa seti 2-0.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ulifanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly Jijini Tanga ambapo wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya TPDC walionekana kuwa makini jambo ambalo liliwawezesha kuibuka na ushindi huo
Baada ya timu hiyo ya wanaume kumaliza kuvuta kamba iliingia upande wa wanawake ambapo timu ya Shirika hilo nayo iliweza kuibuka kidedea baada ya kuwavuta wanawake wenzao wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu (TPHPA) kwa seti 2-0.
Timu ya TPDC ya kuvuta kamba iliwakilishwa vema na wachezaji wake mahiri ambapo kwa upande wa wanaume iliongozwa na Nahodha Joram Ndalahwa,Nnocent Mvamba,Adam Sajilo na Joseph Majebele.
Kwa upande wa timu ya wanawake iliwakilishwa vema na Rehema Saidi,Robi Chambiri,Catherine Madinda na nahodha wao Joyce Kiheka .
0 Comments