NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imelazimishwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya timu ya Mbeya City, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Sokoine Mbeya.
Katika mchezo huo Simba Sc ilianza kupata bao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wao Mzamiru Yasin dakika ya 15 na kuwapelaka mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili klabu ya Mbeya City iliingia ikiwa inahitaji kusawazsiha bao kwani walicheza mpira wa kushambulia bila mafanikio mpaka dakika za lala salama kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Tariq Seif dakika ya 78.
0 Comments