Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWAHIMIZA WATUNZA KUMBUKUMBU KUZINGATIA USIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) kabla ya kufungua Mkutano wa 10 wa Chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 27 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo kwa Wadau mbalimbali waliowezesha kufanikisha Mkutano wa 10 wa Chama cha Menejimenti na Kumbukumbuku na Nyaraka Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 27 Novemba, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) katika picha ya pamoja na Wanachama wa Chama hicho mara baada ya kufungua Mkutano wa 10 wa Chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 27 Novemba, 2022.

Wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) pamoja na Wageni wengine wakimsikiliza mgeni Rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwahutubia kabla ya kufungua Mkutano wa 10 wa Chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 27 Novemba, 2022.

**************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza watunza kumbukumbu kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo ya kiutendaji ndani na nje ya Serikali.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC.

Aidha, Rais Samia amewataka watunza kumbukumbu na nyaraka katika ofisi za umma kutunza siri za Serikali kwa kusimamia maadili ya kazi yao ili kulinda usalama wa nchi.

Vile vile, Rais Samia ametoa wito kwa waajiri Serikalini na sekta binafsi kuhimiza matumizi ya teknolojia kwenye utunzaji wa kumbukumbu na kuimarisha mazingira ya kazi kwa kupunguza mrundikano katika vyumba vya masijala.

Hali kadhalika, Rais Samia amesema matumizi ya teknolojia katika utunzaji wa kumbukumbu utasaidia kurahisisha upatikanaji taarifa zinapohitajika kwa ajili ya maamuzi mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments