NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na ilianzishwa kwa Sheria Namba Mbili (2) ya Bunge ya tarehe 1 Agosti, 2018 baada ya uamuzi wa Serikali wa kuunganisha Mifuko Minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, LAPF na GEPF, lengo likiwa ni kuboresha utoaji huduma na kupunguza gharama za uendeshaji.
MWANACHAMA WA PSSSF
Kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 waliokuwa Wanachama wa mifuko iliyounganishwa yaani PPF, PSPF, LAPF na GEPF waliohamishiwa katika mfuko wa PSSSF wataendelea kuwa wanachama na kuchangia katika Mfuko wa PSSSF.
Aidha Watumishi wapya walioajiriwa kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 katika utumishi wa Umma, mashirika ya umma na makampuni yote ambayo serikali inamiliki zaidi ya asilimia 30 ya hisa watatakiwa kusajiliwa na kuchangia katika mfuko wa PSSSF.
Wanachama wa PSSSF ni pamoja na Wastaafu na Wategemezi waliokuwa wanalipwa pensheni na mifuko iliounganishwa.
Mpaka sasa PSSSF ina jumla ya Wastaafu 150,000 ambao wanalipwa Pensheni ya kila mwezi shilingi bilioni 60.
MAJUKUMU YA PSSSF
Akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari jiji la Dar es Salaam (DCPC), kwenye jengo la PSSSF Jubilee Tower jijini Dar es Salaam Novemba 6, 2022, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Temeke, Bw. Rajabu Kivande ameainisha Majukumu Manne ya PSSSF yaliyotajwa kisheria kuwa ni pamoja na Kuandikisha Wanachama, Kukusanya Michango, Kulipa Mafao, na Kuwekeza kwa mujibu wa Miongozo ya Benki Kuu ya Tanzania ili kulinda thamani ya Michango ya Wanachama.
“Yapo Mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko ikiwa ni pamoja na Pensheni ya Uzee, Pensheni ya Warithi, Pensheni ya Ulemavu, Mafao ya Kukosa Ajira, Mafao ya Uzazi, na Mafao ya Ugonjwa ambao hautokani na kazi,
MAFANIKIO YALIYOPATIKANA
Bw. Kivande alielezea mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuundwa kwa PSSSF mnamo mwaka 2018 baada ya serikali kuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, GEPF NA LAPF.
“Mafanikio makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na kuboreka kwa utoaji huduma kwa Wastaafu na Wanachama wa PSSSF, hivi sasa mstaafu mtarajiwa akikamilisha nyaraka zake zote zinazohitajika, ndani ya siku 60 analipwa Mafao yake kama ambavyo sheria inavyoelekeza.” Amesema Bw. Kivande.
MATUMIZI YA TEHAMA
Kwa nia ya kurahisisha na kuharakisha utoaji wa huduma Mfuko umewekeza kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kupitia PSSSF Kiganjani na PSSSF Popote Ulipo Mtandano.
“Kuna PSSSF Member Portal Mfumo unaomuwezesha Mwanachama na Mstaafu kupata taarifa mbalimbali za Mfuko, Taarifa zake za kibinafsi kama vile Michango anayowasilisha Mwajiri wake, lakini pia kwa Mstaafu anaweza kuhakiki taarifa zake, na kuna PSSSF Billing Portal inayomuwezesha mwajiri kufanya malipo mbalimbali.” Alifafanua Meneja huyo.
UWEKEZAJI
Mfuko umewekeza kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya viwanda, majengo na viwanja vya makazi, alisema Bw. Kivande.
OFISI ZA PSSSF
PSSSF ina mtandao wa Ofisi katika Makao Makuu ya Mikoa yote Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Pia kuna ofisi kwenye baadhi ya Wilaya ambazo kutokana na Jografia yake imeonekana kuna umuhimu wa kuwa na ofisi kwenye maeneo hayo, anasema Bw. Kivande.
Naye Mwenyekiti wa DCPC, Bw. Sam Kamalamo amewashukuru wadau wote walioshirikiana na Klabu hiyo kuwezesha mkutano huo. PSSSF ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa Mkutano.
Meneja wa PSSSF Mkoa wa Temeke, Bw. Rajabu Kivande, akiwasilisha mada mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Klabu ya Waandishi wa Hbaari wa jiji la Dar es Salaam Novemba 6, 2022
Meneja wa PSSSF Mkoa wa Temeke, Bw. Rajabu Kivande, akiwasilisha mada mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Klabu ya Waandishi wa Hbaari wa jiji la Dar es Salaam Novemba 6, 2022
Mwenyekiti wa DCPC, Bw. Sam Kamalamo, akizungumza kwenye mkutano huo.
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Bw. Deo Nsokolo, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtunza Hazina wa DCPD
Makamu Mwenyekiti, Bi. Salome Gregory
Mmmoja wa wajumbe DCPC akizungumza
Mmmoja wa wajumbe DCPC akizungumza
Katibu Mkuu wa DCPC, Bi. Fatma Jalala
Baadhi ya Wajumbe wa DCPC
Baadhi ya Wajumbe wa DCPC
Mwenyekiti wa DCPC Bw. Sam Kamalamo (kulia) akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti, Bi. Salome Gregory
Mmoja wa wajumbe wa DCPC akizungumza kwenye mkutano huo.
0 Comments