*********************
Na Hamida Kamchalla, HANDENI
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameiagiza kuwekwa ndani kwa muda wa saa 24 Ofisa mtendaji wa kata ya Kwamagome, Wilaya ya Handeni Ramadhani Gwalu kwa kutoa taarifa ya uongo ya utekelezaji wa ujenzi shule ya sekondari Togeza.
Agizo hilo amelitia leo katika eneo la ujenzi wa shule hiyo ambapo Gwalu akisoma taarifa yake ambayo ilitofautiana na maelezo baada ya mkuu huyo kumuuliza hakutoa maelezo kama ilivyooandikwa kwenye taarifa.
Aidha Mgumba amesema mahali ilipotakiwa kutumika fedha za mradi hazikuprlekwa na kubadilishiwa matumizi ya eneo ndipo wakapeleka kujenga shule eneo ambalo hata hivyo lina mgogo wa mpaka kati ya Wilaya mbili za Handeni na Kilindi.
"Hapa kuna mgogoro wa mipaka kati ya Wilaya ya Kilindi na Handeni hivyo tunapaswa kusimamisha ujenzi wa shule hii ili kutatua changamoto hiyo na ujenzi wa shule hii ya togeza aijafuata utaratibu,
"Hauna kibali cha Tamisemi na pesa zinazojenga hazikupangiwa hapa
hivyo kuanzia sasa mtendaji wa kata ashikiliwe na jeshi la polisi ilikutoa maelezo ya kwanini ameruhusu ujenzi kuendelea" amesema Rc Mgumba.
Awali akitoa taarifa yake Gwalu alisema shule hiyo ilianza kujenga Octoba 10 mwaka huu ambapo kikao cha kamati ya maendeleo ya kata kilichokutana Octoba 10 na kuazimia shule ijengwe haraka kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kutenbea umbali mrefu.
Alisema muhtasari ulipelekwa kwa Mkurugenzi wa halmashauri, lengo likiwa ni ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, maabara tatu pamoja na vyoo vya walimu na wanafunzi ambao mpaka kufikia jana Novemba 2 kwa hatua iliyofikia umegarimu sh milioni 6.85 ikiwa ni garama za manunuzi ya vifaa mbalimbali na malipo ya ufundi.
0 Comments