***********
Na. Majid Abdulkarim, Dar es Salaam
Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTDS) leo imezindua rasmi zoezi la kampeni ya nyumba kwa nyumba ya ugawaji wa Kingatiba kuthibiti Ugonjwa wa matende na mabusha (Ngirimaji) litakalo tekelezwa katika Halmashauri za Temeke, Kinondoni na Dar es Salaam Jiji.
Zoezi la kampeni hiyo limezinduliwa rasmi na mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni katibu tawala wa Halmashauri ya Kinondoni, BNi. Stella Msofe ambeye amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kuhakikisha wanatokomeza vimelea vya ugonjwa wa matende na mabusha katika mkoa wa Dar es salaam.
Bi. Msofe amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan inajali afya za wananchi na hivyo wamesogeza huduma ya upatikanaji Kingatiba kuthibiti Ugonjwa wa matende na mabusha (Ngirimaji) kuzuia vimelea kusaamba kwa wingi kwani kinga ni bora kuliko tiba.
“Zoezi la utoaji wa Kingatiba kuthibiti Ugonjwa wa matende na mabusha (Ngirimaji) litatekelezwa katika ngazi ya jamii, nyumba kwa nyumba, maeneo mbali mbali ya mikusanyiko kama katika vituo vya magari, shule na masokoni”, ameeleza Bi. Msofe
Afisa Programu kutoka Wizara ya Afya, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTDS), Oscar Kaitaba amesema zoezi hili limekuwa likifanyika mara kwa mara na kuleta matokeo chanya kwa kupunguza na kutokomeza vimelea vya ugonywa wa matende na mabusha nchini.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume amewahamasisha wazazi na walezi kuhakikisha Watoto waliona umri wa miaka mitano na kuandelea wanapatiwa Kingatiba kuthibiti Ugonjwa wa matende na mabusha (Ngirimaji).
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Yondwe amewatoa wasiwasi wanachi kwa kusema kinga inayotolewa ni salama hivyo wajitokeze kwa wingi katika maeneo yao na kupatiwa Kingatiba kuthibiti Ugonjwa wa matende na mabusha (Ngirimaji). MWISHO
0 Comments