Ticker

6/recent/ticker-posts

MAFUNZO KWA WAVUVI YAANZA RASMI MKOANI KAGERA



*******************

NA SHEMSA MUSSA,  KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila amefungua mafunzo ya kukabiliana na maafa hususani kwenye eneo la uokoaji kwa vikundi vya wavuvi kutoka Manispaa ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya Maafa.


Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo ametumia nafasi hiyo kufafanua baadhi ya mambo kuhusiana na ripoti ya ajali ya ndege ya Precision kuwa ipo ripoti ya siku 14, ripoti ya miezi mitatu na ripoti ya baada ya mwaka na kusema kuwa ripoti iliyotolelewa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, chini ya Waziri Profesa Mbalawa ni ya siku 1


Nae Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Moses Machali ameeleza kuwa ujio wa mafunzo hayo ni jambo jema la kupongezwa na yatawajengea uwezo wa namna gani wataweza kukabiliana na majanga pale yanapojitokeza katika maeneo yao.


Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Kanali Selestine Masalamado ameeleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya maafa inajukumu la kusimamia masuala ya maafa Nchini kwa kuzingatia mipango na miongozo kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2004 na Sheria ya Menejimenti ya Maafa Sura namba 6 ya mwaka 2022. Idara imeendelea kupambana kupunguza maafa kwa kusimamia na kuratibu huduma za dharura pale majanga yanapotokea kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi, Idara na Mashirika.


Kutokana na ajali ya ndege ya shirika la precision iliyotokea hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 26 waliokolewa amewapongeza wavuvi walioshiriki katika zoezi zima la uokoaji.


Sambamba na mafunzo, vikundi na wadau wengine wamekuwa na changamoto ya vifaa vya uokoaji ambavyo vinahitajika ili kurahisisha zoezi la uokoaji wa maisha na mali hivyo idara imeona ni muhimu kutekeleza mpango wa kuwajengea uwezo na kuwapatia vifaa vya kisasa kama Waziri Mkuu alivyoelekeza.


Mafunzo haya yatasaidia kutoa huduma kwa haraka na kuongeza idadi ya wataalamu watakaosaidia uokozi baharini na maziwa makuu hivyo kuanzisha vikundi vya uokoaji. Pia yatatolewa kwa vikundi vya wavuvi kutoka Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Muleba.

Post a Comment

0 Comments