Ticker

6/recent/ticker-posts

MAAMUZI HIFADHI YA BONDO KUTOLEWA KESHO, WANANCHI WAOMBA HURUMA YA SERIKALI

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchembe akitoa utambulisho kwa wananchi na meza Kuu aliyokaa mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba pamoja na viongozi wa chama na serikali.
Sehemu ya wananchi wa mtaa wa Bondo wakimsikiliza mkuu wa Mkoa Omari Mgumba akiongea nao kwenye mkutano wa hadhara.


*********************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


HATIMA ya uhalali wa wananchi wanaoishi katika msitu wa Bondo wilayani Handeni pamoja na mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya za Handeni na Kilindi, Mkoa wa Tanga ni kesho Novemba 4, huku wananchi wakiomba huruma ya serikali.


Wananchi hao wametoa malalamiko yao na kusema kuwa wameishi kwenye eneo hilo zaidi ya vmiaka 70 na kwamba wengi wao wameuziwa maeneo na mwenyekiti wa kijiji huku wengine waliotoka Mikoa ya jirani wakiuziwa na wenyeji wao.


"Tumekaa hapa muda mrefu sana, Mimi ni mwenyekti wa Karatu, Arusha, nimekuja hapa nikiwa na watoto wangu watatu mpaka sasa nina wajukuu, tunaomba serikali ituangalie kwa huruma hasa ukiangalia kuna wakina mama na watoto wengi ni kama tutaanza kusumbuliwa na hatumjui kama ni kuhama hapa tutapeleka wapi? amesema Isabela Khaay


"Karibu asilimia 90 ya wananchi tunaoishi Bondo tuko katika eneo hili linaosemekana ni msitu, kwahiyo tunaomba serikali iangaliwe kwa kina jambo hili hiyo siku ya kutoa maamuzi serikali iweze kutuhumia ili tuendelee kuishi kwakuwa sisi siyo wavamizi? amesema Daniel Sulle, mwananchi wa Bondo.


Kuhusu mgogoro wa mpaka wananchi waliopo upande wa Wilaya ya Kilindi wameiomba kupata huduma za kijamii kwakuwa wako mbali sana na sehemu za kutolea huduma hizo kwa upande wa Wilaya yao.


"Ninachoomba ikikupendeza tunaomba Bondo yote ihamie Wilaya ya Handeni kwasababu Songe ni mbali hata huduma za Kiserikali tunazipata kwa shida sana, tunaomba kuhamia huku ili tupate urahisi wa kupata huduma" amesema Sulle.


Akifafanua kuhusu mgogoro huo, mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema mgogoro wa mpaka haugusi wananchi kwakuwa ardhi inalindwa kisheria na serikali hivyo maamuzi yatategemea itakavyoamua lakini pia mpaka haumaanishi kumuhamisha mtu mahali alipo iwe Kilindi au Handeni.


"Hapa Bondo pana kero kubwa sana, Cha kwanza mgogoro wa mpaka kati ya Kilindi na Handeni na kingine kuhusu hifadhi, nataka niwaambieni, mgogoro wa kiutawala ninyi wananchi hauwahusu, wala asitokee kiongozi kuwagombanisha, mipaka hii ni ya sisi viongozi kuonesha wapi kiongozi anaishia katika kuwahudumia wananchi wake" amesema.


"Sioni cha kuchelewesha kutatua migogoro yenu, ifikapo tar 4 mwezi huu kamati za ulinzi na usalama, viongozi wa Ccm pamoja na wataalamu Wilaya zote mbili tukutane ofisi ya mkuu wa Mkoa tumalize tatizo hili na tukishapikea taarifa za wataamu tutakuja kuwaletea majibu mpaka unakuja wapi" amebainisha.


Hata hivyo Mgumba amebainisha kwamba wakazi wengi wanaoishi eneo siyo wenyeji wa asili Bali wamehamia kutoka mikoa mingine lakini kuhama sehemu moja kwenda nyingine haimzuii Mtanzania Bali anapaswa kuishi bila kuvunja sheria za nchi.


"Siyo dhambi, Mtanzania anapaswa kuishi mahali popote ilimradi asivunje sheria, lakini kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa sheria hazijafuatwa, ndiyomaana nikaomba muwe wastahamilivu maamuzi yanakwenda kufanyika" amesisitiza.

Kufuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi hao walioko mpakani kuuziwa maeneo na serikali ya kijiji, mwenyekiti wa mtaa huo amekana ofisi yake kuwajadili na kwamba walijadiliwa na ofisi ya kijiji iliyoko Wilaya ya Kilindi kwani ofisi yake siyo ya kijiji bali ni mtaa.

Post a Comment

0 Comments