Richie Obiri maarufu kama RichieO ameachia kazi yake mpya iitwayo NEW LEVEL ikiwa katika miondoko ya amapiano.
RichieO ni Msanii mwenye Asili ya Nigeria aliyezaliwa nchini Marekani na kukulia nchini Uingereza wakati wa miaka yake ya mapema.
Baadaye alikwenda kuishi nchini Ghana (Afrika Magharibi) kabla ya kurejea Marekani na kufanya makazi ya kudumu.
RichieO alianza kuimba katika kwaya ya kanisa la mtaani na baadae akachaguliwa kuwa kiongozi wa Praise katika sehemu yake ya ibada huko Marekani.
Katika maisha yake yote muziki umekuwa na jukumu muhimu katika maisha yake huku akina Fela Kuti, Sade, Craig David na WizKid wakiwa na ushawishi mkubwa katika sanaa yake Ingawa jumbe za Injili/Inspirational ni maudhui ya nyimbo zake, Afrobeats ndiyo aina anayojieleza vyema zaidi na hivyo Mashabiki wanahaidiwa kazi kubwa toka kwake.
Kwa kuwa karibu na Richieo unaweza kumfuatilia kupitia Twitter @Richieomusik
0 Comments