****************
Wahitimu wa Shahada za awali,Stashahada na Astashahada katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wametakiwa kwenda kutafuta fursa badala ya kusubiri fursa ziwafuate jambo ambalo sio rahisi katika ulimwengu wa Leo.
Ameyasema hayo leo Oktoba 13,2022 Jijini Dar es salaam, Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Prof. William Anangisye wakati wa mahafali ya Hamsini na mbili Duru ya Tatu ya Chuo hicho.
Aidha amewataka wahitimu 2,091 kutambua kuwa elimu haiwezi kuwa chachu ya Mabadiliko yaliyokusudiwa kama haitatumika katika kutatua matatizo katika Jamii.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Balozi Mwanaidi Sinare Majaar amewasisitiza wanataaluma kufanya juhudi Katika kufanya tafiti Kwenye maeneo yatakayogusa maisha ya watanzania Ili ziweze kutoa majibu ya matatizo yaliyopo kwenye Jamii.
Hata hivyo wahitimu hao wamekumbushwa kutosahau kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za utumishi wa umma Katika kuutumikia umma wa watanzania.
0 Comments