Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI MANISPAA YA IRINGA WATAKIWA KUZINGATIA MASLAHI YA WATUMISHI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.

Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.


Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Mohammed Moyo akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa yake, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Mohammed Moyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao wa umma.


Mtumishi wa Iringa Manispaa, Bi. Jamila Mwindi, akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi akisikiliza hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.


Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Philemon Mmbaga (Wakwanza kulia) akichukua taarifa za mtumishi aliyewasilisha changamoto yake wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi aliyoifanya katika halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo.

**********************

Na. Veronica E. Mwafisi-Iringa

Tarehe 27 Oktoba, 2022

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameutaka uongozi wa Manispaa ya Iringa kuzingatia mahitaji na maslahi ya watumishi ili kuwajengea ari na morali ya utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa viongozi wa Manispaa ya Iringa, wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa hiyo akiwa katika ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi hao.

Mimi naomba sana viongozi mbadilike katika suala zima la kusimamia rasilimaliwatu, tuzingatie maslahi na mahitaji ya watumishi wetu ili kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii, weledi na morali ya hali ya juu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka wakuu wa idara katika Manispaa ya Iringa kuwa na utaratibu wa vikao vya mara kwa mara na watumishi wanaowasimamia ili kusikiliza kero zao na kuzitatua kwa wakati.

“Si jukumu la Mkurugenzi au Afisa Utumishi pekee kuzungumza na watumishi, wakuu wa idara mnawajibu wa kuwa na vikao vya kuzisikiliza kero na changamoto zinazowakabili watumishi mnaowaongoza ili kuzitatua,” Mhe. Ndejembi amehimiza.

Kuhusiana na wingi wa malalamiko kutoka kwa watumishi, Mhe. Ndejembi amesema, uongozi wa Manispaa ya Iringa unapaswa kufanya tathmini ya hali ya utendaji kazi kwani idadi kubwa ya watumishi imewasilisha malalamiko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Mohammed Moyo amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kutenga muda wa kusikiliza kero na malalamiko ya watumishi katika wilaya yake ikiwa ni pamoja na kuhimiza uwajibikaji.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amehitimisha ziara ya kikazi Mkoani Iringa iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma.

Post a Comment

0 Comments