Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla amesaini nyaraka za mwisho za makubaliano ya Nchi wanachama wa Baraza kuu la ITU, yaliyoafikiwa kwenye Mkutano Mkuu wa ITU PP22 unaohitimishwa Ijumaa Tarehe 14 Oktoba, 2022 jijini Bucharest, Romania.
Shirika la ITU lilikutanisha Nchi wanachama wake mnamo tarehe 26 Septemba, 2022 ambapo pamoja na majadiliano ya Kisekta, Tanzania ilichaguliwa kuwa miongoni mwa Wajumbe wa Baraza la ITU kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2023 hadi 2026.
Mhandisi Imelda Salum, Meneja wa ofisi ya TCRA Kanda ya Kaskazini, ambaye ameshiriki katika kamati hiyo na kuiwakilisha Tanzania kama Makamu Mwenyekiti Mkuu wa ITU PP22 jijini Bucharest, Romania
Ushiriki wa Tanzania kwenye sambamba na Tanzania kupata nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uhariri wa maudhui yanayojadiliwa kwenye mikutano mbalimbali ya Nchi wanachama, wakati Mkutano Mkuu ukiendelea. Maudhui hayo ndiyo yanayowasilishwa na kupitishwa katika Mkutano Mkuu unaotarajiwa kuhitimishwa Ijumaa Tarehe 14 Oktoba, 2022.
0 Comments