Ticker

6/recent/ticker-posts

TAFITI ZABAINI ASILIMIA 48 YA WATANZANIA WANAUELEWA KUHUSU MAGONJWA YA SARATANI


Tafiti zimebaini kuwa asilimia 48 pekee ya watanzania ndio wenye uwelewa kuhusu magonjwa ya saratani huku wanaume wakiwa na uwelewa wa chini zaidi kwa kuwa na asilimia 16 pekee na wanawake wakiwa wanaelewa kwa asilimia 54.

Hayo yamebainishwa na Dr Harrison chuwa meneja wa mradi mtambuka wa saratani tanzania TCCP kwenye Warsha ya kutoa matokeo ya tafiti za mradi huo ambapo amewataka serikali na wadau kujidhatiti katika Kutengeneza mikakati ya kuongeza uwezo wa maabara na vifaa vya kugundua dalili za awali za saratani katika vituo vya ngazi ya chini vya afya ili kuongeza ufanisi katika matibabu ya saratani.

Kwa upande wake mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza katika mpango wa taifa wa kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kutoka wizara ya Afya DK Anzbet lugakingira amesema serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau na asasi mbalimbali za afya ili kutoa elimu ya ugonjwa wa saratani kwa lengo la kugundulika katika hatua za awali ili jamii iweze kuchukua hatua madhubuti za kuzuia saratani na kuweza kupata matibabu ya haraka

Naye mmoja wa wahanga wa saratani Getrude ndesamburo ameweka wazi kuwa matokeo ya tafiti hizo yatasaidia serikali kupanga mikakati ya kuzuia ugonjwa huo huku akiitaka jamii kufanya vipimo mara kwa mara ili kugundua dalili za awali za ugonjwa wa saratani na kuweza kutibiwa mapema.

Post a Comment

0 Comments