Ticker

6/recent/ticker-posts

NIC , BODI YA USIMAMIZI WA STAKABADHI ZA GHALA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA WA KOROSHO

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye wakisaini mkataba wa makubaliano kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo nchini. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye wakisaini mkataba wa makubaliano kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo nchini. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye wakipongezana mara baada ya kusaini makubalino kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo nchini. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye wakionesha mkataba waliosaini wa makubaliano kutoa huduma za Bima kwenye zao la korosho kwa msimu wa 2022/2023 ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo nchini. Hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu akizungumza katika hafla ya kusaini ya makubaliano na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Oktoba 10,2022 Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye akizungumza katika hafla ya kusaini ya makubaliano na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Oktoba 10,2022 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye wakipata picha ya pamoja na watumishi wa NIC katika hafla ya kusaini makubaliano kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Oktoba 10,2022 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu akizungumza katika hafla ya kusaini ya makubaliano na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Oktoba 10,2022.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) wamesaini mkataba wa makubaliano na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala kutoa huduma za bima katika zao la Korosho kwa msimu wa 2022/2023 ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 10,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC,Dkt. Elirehema Doriye amesema wameamua kuingia makubaliano hayo ili kutatua changamoto katika ununuzi wa zao la korosho nchini.

Amesema Bima hiyo itahusisha kulipa gharama za ajali ya moto zitakazokuwa zinatokea maghala ambapo awali wakulima na wafanyabiashara wa zao la korosha walikuwa wanapata changamoto kutokana na baadhi kutokuwa na bima ya mazao yao.

“Zao la korosho lilikuwa na changamoto kidogo, NIC kwa kutekeleza sera za serikali tumetafuta suluhisho ili ununuzi wa korosho usiwe na hasara au changamoto,”Amesema Dkt.Doriye.

Aidha Dkt.Doriye amesema NIC imepunguza siku za kulipa madai kutoka siku saba, hadi nne ikiwa ni sehemu ya kufanya maboresho katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Asangye Bangu, amesema makubaliano hayo yataimarisha utendaji wa mfumo wa Stakabadhi za Ghala nchini kwa kuondoa kero ya malipo kwa wanunuzi baada ya kukosa mzigo kamili ghalani.

Pamoja na hayo ,Bw. Bangu amewataka wanunuzi wote nchini kuhakikisha hawafanyi uzembe wa makusudi wakitegemea kuna bima ambayo wamekata kwani wakifanya hivyo watajiondolea uaminifu.

Amesema baada ya kutolewa kwa bima hiyo bodi itafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara katika maghara na hata hivyo katika kipindi cha mwaka huu kampuni 20 zitaenda kunufaika na bima hiyo.

Post a Comment

0 Comments