Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akizungumza katika Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Uhandisi wa Mitambo na Viwanda lilofanyika leo Oktoba 20,2022 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akizungumza katika Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Uhandisi wa Mitambo na Viwanda lilofanyika leo Oktoba 20,2022 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma), Profesa Bonaventure Rutinwa akizungumza katika Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Uhandisi wa Mitambo na Viwanda lilofanyika leo Oktoba 20,2022 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Rasi wa Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia Prof. Bakari Mwinyiwiwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Uhandisi wa Mitambo na Viwanda lilofanyika leo Oktoba 20,2022 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akipata picha ya pamoja na wadau wa elimu nchini katika Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Uhandisi wa Mitambo na Viwanda lilofanyika leo Oktoba 20,2022 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga akipata picha ya pamoja na wadau wa elimu nchini katika Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Uhandisi wa Mitambo na Viwanda lilofanyika leo Oktoba 20,2022 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Serikali ipo mbioni kuja na Sheria na Sera mpya ya Elimu nchini ambayo inatazamiwa kuzinduliwa Desemba mwaka huu ambapo katika sera hiyo mapinduzi ya mtaala wa elimu yatafanyika kuanzia shule za awali, sekondari O level, A level na Vyuo lengo ni kuhakikisha Taifa linakuwa na wahitimu watakaoweza kujiajiri na siyo kuajiriwa pekee.
Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 20,2022 Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga wakati wa Uzinduzi wa Kongamano la Kimataifa la Uhandisi wa Mitambo na Viwanda lilofanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
" Hadi sasa Serikali kupitia Wizara ya Elimu imeshaanza kupitia sheria ya elimu ya mwaka 2014, Sera ya elimu ya mwaka 1978 na mitaala ya elimu ili kufanya maboresho yatakayowawezesha wanafunzi mbali na kusoma kwa nadharia pia watafundishwa kupata ujuzi katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufundishaji wa ujasirimali". Amesema
Akielezea lengo la kongamano la 7 la kimataifa lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rasi wa Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia Prof. Bakari Mwinyiwiwa amesema kongamano hilo litawasaidia wahandisi wa vyuo kushirikiana na wahandisi wa viwandani kufanya kazi zao kwa weledi, na kuleta maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
0 Comments