Ticker

6/recent/ticker-posts

MOI YAOKOA ZAIDI YA SH.MIL 180 KWA KUFANYA UPASUAJI NA KUREKEBISHA VIUNGO VYA WATOTO 10


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili-MOI, imeokoa zaidi ya Shilingi Milioni 180 baada ya kushirikiana na wataalamu kutoka nchini Ireland ambao waliweka kambi nchini kwa kufanya upasuaji wa kurekebisha viungo kwa watoto 10.

Akizungumza leo Oktoba 27,2022 na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI,Dkt. Respisius Boniface amesema kumtibu mtoto mmoja nje ya nchi unagharimu kiasi cha shilingi milioni 20 hadi kufikia milioni 30 wakati akiffanyiwa matibabu hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingi milioni 1.3 hadi milioni 3.

Aidha Dkt.Boniface amesema kupitia kambi hiyo wameweza kunufaika kwa wataalamu wao ambao wameweza kupatiwa mafunzo ya kutosha na kuletewa mashine tiba ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya matibabu katika taasisi hiyo.

“Kambi hii ya matibabu ilianza jumatatu na kumalizika leo hii ni katika kuanzisha ushirikiano na wenzetu wa Ireland ambapo faida tulizopata Kwanza ni kambi ya matibabu na mafunzo kwa wataalmu wetu, tiba kwa wagonjwa wetu,wameleta mashine tiba na wataalamu wetu watakuwa wanatoka hapa kwenda Ireland kwa Mafunzo ya muda mfupi ili kuongeza ujuzi,”Amesema Dkt. Boniface.

Pamoja na hayo amesema kuwa wataalamu hao kutoka nchini Ireland wamewaletea mashine tatu ambazo zinasaidia kurahisisha shughuli na vipandikizi vyote hivyo vina gharama ya shilingi milioni 117 .

Kwa upande wake Daktari Mbombezi wa Magonjwa ya Mifupa na Uti wa Mgongo, Dkt.Antony Asey amesema kupitia kambi hiyo wamejifunza mbinu mpya ya upasuaji ambao haujafanyika kabla.

”Kikubwa ambacho tumejifunza kipya kwa upasuaji wa uti wa mgongo kuna baadhi ya magonjwa uzoefu wetu katika kutibu magonjwa hayo bado ulikuwa sio mkubwa mfano ugonjwa wa baridi ya bisi pamoja na kutokea katika mifupa mikubwa ,magoti na vidole vya miguu na nyonga lakini pia inatokea kwenye uti wa mgongo.

Aliongeza “Sanasana kwenye sehemu ya juu ya shingo pale mbapo inaungana na kichwa hao wanapata matitizo ya mfumo mzima wa fahamu wanapoteza nguvu ,uwezo wa kutembea na Kubwa ambacho tumengalia katika upasuaji huu ni mbinu mpya ya kufanya upasuaji katika eneo hilo ambalo limejificha kuna misuli mingi kwenye shingo sasa tunaweza kufanya matibabu ya kuweka vyuma na waya". Amesema

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Saidizi Dkt. Asha Said amesema wameweza kubadilishana ujuzi katika kutoa dawa ya usingizi kwa watoto hasa dawa za block ambazo walikuwa wanawapa watu wazima tu.

Madaktari Bingwa wa Mifupa wakiendelea na ubasuaji kwa mgonjwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) leo Oktoba 27,2022 Jijini Dar es SalaamMkurugenzi Mtendaji wa MOI,Dkt. Respisius Boniface akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27,2022 baada ya kumalizika kwa kambi ya upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchini Ireland.

Post a Comment

0 Comments