NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Mchakato wa kumpata Mshindi wa Mashindano ya Wanamitindo na warembwende wa Dunia umeanza ambao Watanzania wametoa ahadi ya kubakisha ushindi Nyumbani.
Akizungumza kuelea Shindano hilo ambalo linatarajia kufanyika Oktoba 29,2022 Jijini Dar es Salaam, Mrembwende Khadija Rajabu amesema wamejipanga ipasavyo licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo lakini imani yao ni kushinda na kubakisha taji nchini.
Aidha amesema amejipanga vizuri na anaamini ataipeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika Mashindano hayo ya dunia.
Kwa upande wa washiriki wengine kutoka mataifa mengine wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa mashindano hayo kuwa huru.
0 Comments