Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKALA YA WIKI LA VIJANA MKOANI KAGERA PAMOJA NA KILELE CHA KUZIMA MWENGE WA UHURU 2022.


Mjasiriamali Saimon Sirilo.


Kwa kushirikiana na Shirika la Restless Development linalofanya kazi na Vijana tumeshiriki katika maadhimisho ya wiki la vijana na kuweza kubadilishana mawazo na vijana wengi wa Kitanzania mkoani kagera kwa kuwajengea uwezo katika mambo kadhaa ikiwemo namna ya kujiajiri,Afya na makuzi pia.

Kupitia mambo mtambuka yanayowahusu kujenga uchumi wa vijana nilifanikiwa kuwa moja ya wanajopo walioendesha mdahalo uliojikita katika kuzungumzia hatma ya uchumi wa vijana kupitia mafaniko,changamoto na mapendekezo kwa serikali.

Binafsi,nilitoa mawazo yangu kama ifuatavyo

1:Vijana kuwa na uthubutu na kuanzisha mambo/miradi japo kwa kidogo ili kuweza kuiaminisha serikali kuwa vijana tunao uwezo,maarifa,nguvu na ari ya kufanya kazi...hapa ndipo serikali itawashika mikono kupitia zile fedha asilimia 4 za vijana kutoka halmashauri.

Uthubutu huleta kuaminika zaidi kuliko maneno matupu,kijana mwenye uthubutu huaminika zaidi kuliko asiyeanza kabisa.

2: Vijana tujitahidi kutafsiri fursa zinazotuzunguka katika jamii zetu ili kuifanya serikali ione fursa hizo zina tija katika jamii zetu na kutupatia fedha kama mtaji.

Fursa zipo nyingi sana ila zinapaswa kutafsiriwa kwa umuhimu wake, mfano, jamii moja inaweza ona fursa zaidi ya moja kwa kitu kile kile...Mti waweza kuwa na fursa nyingi kadiri atakavyoutafsiri mtu,mwingine anaona mti ni fursa ya mbao, mwingine fursa ya dawa,mwingine fursa ya kiganga,mwingine fursa ya mazingira nk...hivyo ukienda kwa hoja hii ya tafsiri na kuelezea faida yake utaaminika zaidi.

Fursa zipo nyingi sana ila zinapaswa kutafsiriwa kwa umuhimu wake na hapa ndio hoja ya kusema vijana tubadili taaluma zetu kuwa fedha na ziendane na matumizi ama mahitaji ya jamii husika.

*Changamoto zinazowakabili vijana na kushindwa kufikia malengo yao*

1: Ukosefu wa mtaji,hii ni kutokana na kutumia muda mwingi masomoni na kurudi mtaani wakiwa hawana kitu kabisa.

2: Jamii kuwa na kasumba y kutowaani kulingana na sifa za vijana wachache kutoridhisha.

3: Vijana wasomi wamejengewa uwezo wa kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri,jambo hili huwapa changamoto vijana pale wanapokosa ajira walizozisotea kwa muda mrefu.Vijana wengi hujikatia tamaa ya kupambana baada ya kukumbana na ugumu wa maisha.

*Mapendekezo*

1:Vijana waanzishe mawazo na kuunda vikundi wakapewe fedha halmashuri pamoja na mfuko wa vijana kutoka wizara inayohusika na vijana na watu wenye ulemavu ambapo hata kijana mmoja mmoja huweza kukopesheka kwa masharti nafuu.

2: serikali iwaamini vijana na kuendelea kutengeneza miundombinu wezeshi ili kuwawezesha vijana kufikia malengo yao.

3: serikali ibadili mfumo kwa wasomi wanaopata fedha za mkopo kwaajili ya masomo yao basi ikifaa kiasi kidogo cha asilimia anachopata mnufaika basi atunziwe ili punde amalizapo masomo yake akabidhiwe fedha yake na iwe kama kiinua mgongo cha kumsaidia kuanza biashara wakati akisubiria ajira na hii itamsaidia kuanza kurejesha huo mkopo aliopewa chuoni.

Mfano, kama mtu amepewa mkopo asilimia 100 basi wakati wa masomo yake akabidhiwe asilimia 80 kwa mwaka na asilimia 20 aitunziwe kila mwaka ili amalizapo masomo yake akabidhiwe ili iwe kama mtaji wake wa kuanzia maisha wakati anasubiria ajira yake kwani serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi sana kwa wanafunzi lakn hazirudi kutokana na vijana hao kukosa ajira.

*Mwisho*

Sisi vijana tunaendelea kupambana na kujengeana uwezo sisi kwa sisi, pia tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita chini ya mama samia kwa mambo makubwa inayofanya kwa vijana kwa mustakabali wa Taifa letu na tupo bega kwa bega na Mh. Rais kuhakikisha tunalijenga Taifa letu pendwa.

Imeandaliwa na SAIMON SIRILO

MJASIRIAMALI

Post a Comment

0 Comments