Ticker

6/recent/ticker-posts

KITUO CHA POLISI CHAKOSA USAFIRI, WATUTUMIWA WAKODISHIWA BODA NA WALALAMIKAJI.


***********************

Hamida Kamchalla, KILINDI.


WANANCHI kata ya Negero, Wilaya ya Kilindi wameiomba serikali kuwaondoa katika hali ya kuhujumiwa katika kesi za jinai kwakuwa mtu akifungua kesi hizo anatakiwa kuwajibika kumsafirisha mshtakiwa wake kwenda mahakamani.


Wametoa Rai hiyo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kwenye mkutano wa hadhara na kusema hali hiyo imekuwa kero kubwa kwao kwani wengine wanaonelewa na hawana uwezo wa kumsafirisha mshtakiwa wake kutoka Negero hadi makao makuu ya Wilaya (Songe).


"Mtu unafanyiwa uhalifu, unarupoti na kesi inafunguliwa inafika kipindi mshtakiwa kupelekwa kule makao makuu ya Wilaya ambako ndiyo kwenye mahakama,


"Unaambiwa ukodishe pikipiki mbili ili mshtakiwa na msindikizaji wapande moja na mlalamikaji nae apande yakeakini pikipiki hizo zinakodishwa moja sh elfu 60 kwenda na kurudi kwahiyo hapo jumla ni sh laki moja na elfu 20" alisema Ezron Kinasa.


Aidha Kinasa amebainisha kwamba mbali na malalamiko hayo lakini hawana sababu ya kuwalaumu askari katika kata hiyo kwakuwa hawana gari la kubebea watuhumiwa kuwapeleka mahakamani.


"Tunaomba utusaidie mheshimiwa mkuu wa Mkoa, hii kazi ya kusafirisha watuhumiwa wa makosa ya jinai anahusika nani,


"lakini pia naomba kwa niaba ya hawa askari ufanye kila linalowezekana uwapatie gari pale kituoni ili waweze kusafirisha mahabusu wao wenyewe, tunajua kwa mamlaka uliyopewa unaweza kuongea na ngazi za juu na gari ikapatikana hapa" alisisitiza.


Naye mkuu wa Mkoa amekiri kuwa kituo hakina gari na kusema kuwa amelichukua suala hilo na atakwenda kufifnyia kazi kwa kushirikiana na viongozi wengine ngazi za juu serikali na kulifanyia kazi.

Post a Comment

0 Comments