Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA WESE YAJA NA SULUHISHO LA MTAJI KWA VIJANA WA BODABODA NA BAJAJI



*********

Na Magrethy Katengu 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam Godwin Gondwe amewashauri vijana kuachana na kuwa tegemezi huku wakijilamu hawana mitaji wajichanye na Kampuni zinazojihusisha kutoa mikopo katika nyanja mbalimbali ikiwemo mabenki.

Ushauri huo umetolewa leo Dar es salaam kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa uzinduzi wa jukwaa la kutoa huduma ya mafuta nakulipa baadae lililoanzishwa na kampuni ya WESE, Gondwe amesema kuwa jukwaa hilo litawasaidia vijana wanaopata vyombo vya moto kama bajaji na pikipiki kupata mtaji wa mafuta nakulipa baadae bila kuwepo na riba.

Alisema kuwa wazo la WESE kubuni jukwaa hilo litakalotumika kutoa huduma ya mafuta kwa kuunganisha madereva na vituo vya kuuza mafuta kwa kutumia utaratibu wa kununua-sasa na lipa baadae utasaidia vijana wengi ambao watafanya shughuli za kuwaingizia kipato nakuaminika kwenye taasisi za kifedha kama vile mabenki.

"WESE mmekuja na teknolojia hii ambayo malengo la kupaisha vijana wa Daresalaam hususani madereva wa bajaji na bodaboda, pamoja na kuwatambulisha kwa kazi wanazozifanya kwani wanaweza kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha ikiwemo mabenki kutokana na wao kuaminiwa" alisema DC Gondwe.

Alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiweka mazingira wezeshi kwa vijana kujipatia ajira nakuendesha maisha yao hivyo Kampuni ya WESE imeunga mkono jitihada za serikali kwa kuanzisha jukwaa hilo la kutoa mtaji wa mafuta kwa vijana ambao wanapata vyombo vya moto kama vile bajaji na pikipiki.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Jukwaa hilo Frances Ekeng alisema kwamba kuanzisha jukwaa hilo ni kushirikiana na sekta ya uchukuzi nchini Tanzania ambayo inakuwa kwa kasi nakwamba ni mojawapo ya waajiri wakubwa wa wafanyakazi kwa sababu ya nafasi yake ya kimkakati katika uchumi wa Taifa.

Hata hivyo kwamba madereva wadogo wa kibiashara wanakabiliwa na hali duni ya maisha ambapo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya madereva nchini Tanznia hawamiliki vyombo vya usafiri wanavyoendesha lakini mara nyingi wanatarajiwa kuwajibika kwa natengenezo madogo hadi makubwa , mikataba ya kazi na mabosi wao ,kutokuwa na uhakika wa ajira,ukosefu wa bima.







Changamoto zingine ni mabadiliko ya soko katika kushuka na kupanda kwa bei ya mafuta duniani,hivyo pamoja na hayo sekta ya fedha imekuwa haiwaamini vya kutosha madereva wadogo wa kubiashara kwa mikopo midogo midogo ili kusimama ustawi wao wa kila siku, hivyo WESE imetambua changamoto hizo nakubuni jukwaa hilo ili madereva wapate huduma za mafuta na kulipa baadae.

Post a Comment

0 Comments