Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA AGRICOM YATUMIA MASHINDANO YA SHIMIWI KUTOA ELIMU

i




Na Oscar Asssenga, Tanga,


AFISA Masoko kutoka Kampuni ya Agricom inayojihusisha na uuzaji na usambazaji wa zana za kilimo Baraka Konkara amesema wametumia mashindano ya Shirikisho la michezo ya idara, wizara na taasisi za serikali (SHIMIWI) kutoa elimu na kuwahamasisha watumishi wa umma namna ya kuweza kujiajiri katika kilimo ili hata wanapostaafu wawe na shughuli ya kuwakwamua kiuchumi.


Baraka aliyasema hayo wakati wa ufungaji wa mashindano ya 36 ya Shimiwi yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Tanga.


Alisema kuwa serikali imekuwa ikiweka jitihada kubwa katika suala zima la kilimo hivyo basi na wao wamekuwa sehemu ya kuweza kuunga mkono ile agenda ya wizara ya kilimo.


Alisema kilichowavutia zaidi kuweza kudhamini mashindano haya kwanza kabisa ilikuwa inakosa ufadhili hivyo basi tumekuwa kwa kipindi cha miaka miwili ikiwemo mwaka jana na mwaka huu wamedhamini mashindano hayo lakini wanaona katika udhamini wa mashindano hayo wanaweza kuwasaidia wenzao wa serikali ambao ni wadau muhimu sana ili waweze kufanikisha michezo katika kuboresha afya zao na kujenga mahusiano mazuri kazini.


Alisema kwamba licha ya kuwajua watumishi hao wa Umma lakini pia wamekuwa wakijihusisha na shughuli nyingine za kujiingizia kipato ikiwemo za kilimo jambo ambalo limewasukuma kudhamini mashindo hayo kwa lengo la kuwaweka karibu na kuwapa mbinu za kilimo chenye tija kinatachowakwamua na umasikini.


Konkara amesema kuwa watahakikisha wanaendelea kuangalia ni namna gani wanavyokuwa na ukaribu na watumishi hao wa umma katika suala zima la mikopo ambayo inakuwa na riba nafuu kwa kushirikiana na mabenki mbalimbali.


"Lengo letu ni kuweza kuwafikia popote pale walipo ili pia wanapostaafu wawe na shughuli nyingine za kufanya baada ya kustaafu wasije wakawa wanaingia mtaani wakawa wageni zaidi kwahiyo tunawahudumia zana hizi za kisasa za kilimo na kuwapatia unafuu mkubwa ambao maeneo mengine wanashindwa kupata, "alisisitiza Konkara.


Awali akizungumza wakati akifungua Mashindano hayo ya Shimiwi, Mkuu wa Mkoa Tanga Omari Mgumba aliipongeza kampuni hiyo ya Agricom kwa kuwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo jambo ambalo linapaswa kuigwa na makampuni mengime huku akiwataka watumishi hao wa umma kuendelea kutenga muda wa kufanya mazoezi katika sehemu zao za kazi.


Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka watakaporudi kwenye sehemu zao za kazi kuhakikdha wanaendelee kufanya mazoezi kama sehemu ya maisha .


Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka pia waende kujiandaa kwa ajili ya mashindano ya mwaka ujao huku akiwataka wakawe mabalozi wazuri kuwahimiza wenzao ili mwaka ujao wanatekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais ya kuhakikisha wanachama wote wanaoshiriki kwenye michezo hii wanatimiza azma ya serikali ya kuwashirikisha watumishi wote kufanya mazoezi na kushiriki kwenye mashindano.

Post a Comment

0 Comments