Ticker

6/recent/ticker-posts

JIJI LA TANGA LAWAITA WAWEKEZAJI

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusu fursa za uwekezaji katika Jiji hilo na namna walivyojipanga kupokea wawekezaji ambao watafika.


*******************

Na Oscar Assenga,TANGA.


HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imewaita wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo kutokana na uwepo wa maeneo yanayotosha kwa ajili ya viwanda hasa sekta mbalimbali ikiwemo ya Madini.


Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu fursa za uwekezaji katika Jiji hilo na namna walivyojipanga kupokea wawekezaji ambao watafika.


Aliyataja maeneo ambayo yanafaa kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya Madini katika Jiji hilo yapo katika eneo Maere,Chumvini,Kisosora,Ndaoya,Machui,Tongoni, Chongoleani,Mwarongo.


Dkt Sipora alisema katika maeneo hayo yana hekta 212 na yanafaa kwa ajili ya maeneo ya viwanda vya saruji,chokaa,chumvi pamoja na rangi kwamba sababu chumvi inayozalishwa inatumika uzalishaji bidhaa mbalimbali hivyo wanatangaza na kualika wawezekezaji wafika kwa ajili ya viwanda.


"Katika maeneo ya madini tunawaalika wawekezaji wakubwa na wadogo wa Madini na chumvi hivi sasa uzalishaji ni mdogo sana unakuta wazalishaji wadogo wadogo wanazalisha kama tani 6000 hazitoshi hivyo tunawaalika kuja kuwekeza na tumehaidi hakutakuwa na urasimu wa kupata maeneo hayo ambayo tayari yameshapimwa"Alisema Dkt Sipora.

Alisema pia katika maeneo hayo yanayofaa kwa ajili ya sekta ya uvuvi yaani uchumi wa bluu kutokana na uwepo wa bahari hivyo kuna fursa ya kufanya uvuvi na kuwaalika wawekezaji wanaoweza kuja kuingia meli kubwa na boti kwa ajili ya kufanya uvuvi.


"Lakini pia unenepeshaji wa magongoo bahari,kilimo cha mwani hao wote tunawaita lakini pia ufungaji wa samaki kwenye vizimba na uvuvi wa kutumia vyombo vya kisasa" Alisema


Alisema wameamua kuwaita wawekezaji hao kwa ajili ya shughuli za uwekezaji na viwanda ambavyo ni muhimu sana huku akieleza Rais Samia Suluhu ametangza ameifungua nchini na kuiunganisha nchi na masoko nje ya nchi hivyo kilichobakia ni wana Tanga waongeza uzalishaji ku
uza nje ya nchi na zile zilizopo kwenye bara la Afrika


"Tunapokuwa na viwanda inasaidia kuchukua nguvu kazi ya vijana ,twaliopo baada ya kilimo wanakuwa hawana cha kufanya kwa hiyo wote watapata ajira kwenye viwanda ambavyo vitaongeza thamani na muda wa kuishi kwa bidhaa husika kwa mfano unaposafirisha machungwa yanaweza kuozea njiani lakini wanapounguza gharama za kusafirisha na kukuta nafasi kubwa inchukuliwa kwenye gari na bidhaa nyengine zinaharibikia njiani hivyo kupunguza upotevu wa mazao na kuongeza thamani ya mazao" Alisema Mkurugenzi huyo.


Aidha aliwataka wawekezaji ambao wanakwenda kuwekeza Visiwani Zanzibar kupitia uchumi wa bluu waona namna ya kugawana na wengi wake Jijini Tanga ambako mako kuna fursa ya uwekezaji huo ambao ni muhimu kwa maendeleo.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments