Ticker

6/recent/ticker-posts

IKUPA TRUST FUND, BARRICK WATOA MSAADA WA VITI NA KITANDA CHA KUJIFUNGULIA WATU WENYE ULEMAVU KAHAMA

 

Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu (katikati) na Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Sekondo (kushoto)  wakikabidhi kitanda cha kujifungulia kwa ajili ya wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, wametoa msaada wa viti mwendo vitano kwa ajili ya watoto wenye ulemavu na kitanda maalumu cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.


Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVep) inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation,Mark Bristow, akiwa nchini hivi karibuni alikabidhi msaada wa dola 10,000 kwa taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za wanawake wenye ulemavu.


Msaada huo umekabidhiwa wilayani Kahama leo Alhamisi Oktoba 13,2022 na Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu.


Akizungumza wakati wa kukabidhi viti na kitanda hicho vyenye thamani ya shilingi Milioni 3.1, Mhe. Ikupa amesema Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wanatambua mchango watu wenye ulemavu katika jamii hivyo ni lazima wapate huduma kama wanavyopata watu wasio na ulemavu.


“Tunaungana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza kuwepo vyumba maalumu vya kujifungulia kwa watu wenye ulemavu. Wakati wa kujifungua watu wenye ulemavu wanapata changamoto nyingi ukilinganisha na watu wasio na ulemavu. Watu wenye ulemavu tunahitaji usiri na miundo mbinu rafiki wakati wa kujifungua ndiyo maana tumeona umuhimu wa kuleta kitanda cha kujifungulia kwa watu wenye ulemavu”,amesema Mhe. Ikupa.


“Naomba jamii iwaone watu wenye ulemavu ni kama watu wengine wasio na ulemavu. Kuwa na ulemavu siyo jambo la ajabu. Jamii ione suala la kuoa au kuolewa ni la kawaida. Jamii ituone sisi watu wenye ulemavu wanaume au wanawake tuna haki ya kuoa au kuolewa na kupata watoto maana kuna wengine wanashangaa kuona mtu mwenye ulemavu ana ujauzito na kuwa na mitazamo hasi kwamba waliowapa ujauzito wanawatesa, jambo ambalo siyo kweli. Sisi pia tuna haki ya kuzaa”,ameongeza Mhe. Ikupa.


Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu aliyeiwakilisha kampuni katika hafla hiyo, Bi. Zuwena Sekondo amesema Kampuni ya Barrick na Ikupa Trust Fund wametoa viti kwa ajili ya watoto wenye ulemavu na kitanda maalumu cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu ili kuwapa furaha watu wenye ulemavu na kuwaonesha kuwa wanaweza kufanya kazi na kuzalisha kwa tija kama watu wengine wasio na ulemavu.


Naye Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake na Watoto wenye ulemavu Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Rehema Joshua ameishukuru Ikupa Trust Fund na Barrick Bulyanhulu kwa msaada huo huku akisisitiza kuwa watu wenye ulemavu wana haki ya kupendwa, kuoa, kuolewa na kupata watoto kama watu wengine.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Dkt. Deo Nyaga amesema kitanda hicho cha kujifungulia watu wenye ulemavu kitasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha utoaji huduma kwa wanawake wenye ulemavu na kwamba pindi ujenzi wa jengo la akina mama na watoto litakapokamilika watakuwa na chumba maalumu cha kujifungulia akina mama wenye ulemavu.

Akiwa wilayani Kahama, Mhe. Ikupa amezindua jengo la darasa la wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya Danviva English Medium.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya viti na kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama vilivyotolewa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya viti na kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama vilivyotolewa Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick.
Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya viti na kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama vilivyotolewa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick.
Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Sekondo  akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya viti na kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama vilivyotolewa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick.
Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Sekondo  akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya viti na kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama vilivyotolewa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick
Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu (katikati) na Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Sekondo (kushoto)  wakikabidhi kitanda cha kujifungulia kwa ajili ya wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu (katikati) akishikana mkono na Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Sekondo (kushoto)  wakati wakikabidhi kitanda cha kujifungulia kwa ajili ya wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu (wa tano kutoka kulia) na Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Sekondo (kushoto)  wakikabidhi viti vitano kwa ajili ya watoto wenye ulemavu Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu (wa tano kutoka kulia) na Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Sekondo (kushoto)  wakikabidhi viti vitano kwa ajili ya watoto wenye ulemavu Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Watoto wenye ulemavu Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga wakiwa wamekaa kwenye viti vilivyotolewa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick.
Muonekano wa sehemu ya viti vilivyotolewa na  Ikupa Trust Fund na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wilayani Kahama
Kaimu Meneja wa Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Zuwena Sekondo (kushoto) akizungumza jambo na Mwanzilishi wa Ikupa Trust Fund Mhe. Stella Ikupa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia makundi ya watu wenye ulemavu.
Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake na Watoto wenye ulemavu Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Rehema Joshua  akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya viti na kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama vilivyotolewa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Dkt. Deo Nyaga  akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya viti na kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama vilivyotolewa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick
Wadau wakiwa katika hafla fupi ya makabidhiano ya viti na kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu katika hospitali ya wilaya ya Kahama vilivyotolewa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, akikabidhi vocha ya Dola za kimarekani 10,000 kwa Meneja Miradi wa taasisi ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles kwa ajili ya kusaidia miradi ya akina mama na watoto wenye ulemavu alipofanya ziara ya kikazi nchini hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments