***********
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeendeleza na rekodi yake ya kutokufungwa katika mechi ya 44 mara baada ya leo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC Fc.
Yanga Sc imeingia uwanjani huku ikiwapumzisha wachezaji wake kadhaa akiwemo Mayele ambaye hakuwepo hata benchi, Feisal Salum ambaye aliingia na kufunga bao dakika ya 80 na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi, Moloko ambaye aliingia kipindi cha pili pamoja na Aucho ambaye nae hakuwepo hata benchi.
Katika kipindi cha kwanza timu zote hazionesha zilishambuliana japo mpira ulikuwa unachezwa katikati ya uwanja.
0 Comments