*******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Azama Fc imefanikiwa kuinyuka Simba Sc bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Bao la Azam Fc lilifungwa na Prince Dube ambaye alipachika bao kali ambalo lilifungwa katika kipindi cha kwanza.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake, licha ya Azam Fc kukosa nafasi za wazi wamefanikiwa kuondoka na ushindi huo kwa mara ya kwanza tokea mwaka 2017 dhidi yao Simba Sc.
0 Comments