Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI MKOA WA MWANZA WATAKIWA KUTEMBELEA VIVUTIO

Afisa uhifadhi wa wanyamapori daraja la pili kutoka hifadhi ya Taifa kisiwa cha saa nane Hilda Mikongoti akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 17 ya Afrika mashariki.

*********************

Na SHEILA KATIKULA,MWANZA

Wananchi mkoani Mwanza wametakiwa kujitokeza kutembea vivutio vya utalii vinavyopatikana mkoani hapa.

Hayo yamebainishwa leo na Afisa uhifadhi wa wanyamapori daraja la pili kutoka hifadhi ya Taifa kisiwa Cha saanane mkoani Mwanza Hilda Mikongoti wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 17 ya Afrika mashariki yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza.

Mikongoti amesema kuwa wananchi wajitokeze kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi hiyo

" Ninawaomba na kuwakaribisha watanzania wote kuja kupata elimu na kujua vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania waje kwenye banda letu la mali asili na mtu akifika atapata taarifa ya kujua jinsi ya kutufikia na gharama zake za kutufikia katika hifadhi ya kisiwa cha saanane"amesema Mikongoti.

Hata hivyo maonyesho hayo ya 17 ya wafanyabiasha Afrika Mashariki yanayofanyika katika viwanja vya Nyamagana kuanzia agosti 26 mwaka huu nayatarajia kumalizika Septemba 4 ambayo yanayohusisha nchi takribani nane ikiwemo Tanzania,china,Uganda,India,Rwanda,Burundi, Kenya na Indonesia ambayo yameandaliwa na chemba ya wafanyabiasha wenye viwanda,kilimo na biashara (TCCIA).

Post a Comment

0 Comments