Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uendelezaji milki nchini uliofanyika leo Septemba 1,2022 jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dkt.Allan Kijazi akizungumza katika Mkutano wa wadau wa uendelezaji milki nchini uliofanyika leo Septemba 1,2022 jijini Dar es Salaam.
*********************
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula amepiga marufuku kwa wapimaji na waendelezaji wa Milki kuuza viwanja vyenye vipimo vidogo kinyume cha maadili na atayebaina atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.
Agizo hilo ameitoa leo katika kikao cha wadau wa Ardhi (Milki) jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa tokea kuwepo kwa ongezeko la kampuni za uuzaji wa Ardhi kumekuwa na wimbi la uuzaji holela wa maeneo maarufu kama ishirini kwa ishirini ikiwa ni pamoja na kuuza maeneo mara mbili kwa watu tofauti na kuzalisha migogoro baina ya jamii.
Ameongeza kuwa sekta ya Aridhi na miliki imekuwa ikikabikiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa nyumba bora na gharama nafuu takwimu zilizopo nchini zinaonyesha kuwa kwa mwaka kunatakiwa kujengwa nyumba 200,000 lakini nyumba zilizojengwa ni 13,837.
"Kasi ya ujenzi nyumba ni ndogo mno ukilinganisha na kasi ya ongezeko la watu hivyo washiriki kwa kuzingatia changamoto tulizonazo ili tujadili kwa pamoja na kutafuta suluhu ya changamoto hizo mijini na vijijini,tusiangalie mijini tu,tukiwekeza hususani vijijini kwa kupanga vizuri maeneo" Alisema Mabula.
Aidha Dakta mabula amezitaka taasisi za kifedha hususani Bank nchini kutafuta njia nzuri zaidi ambayo itarahisisha utoaji ww mikopo yenye riba nafuu kwa wananchi katika ujenzi wa nyumba nchini ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo ya urasimishaji wa Ardhi ambapo zoezi hilo litakamilika 2023.
Kadhalika amesema Taasisi zinazojihususha na uendelezaji milki uzingatie ujenzi wa kijani kwa kujenga na kuacha nafasi ya upandaji miti na maua.
"Kwa sasa kibali cha ujenzi wa nyumba ya makazi ni lazima kuwepo na nafasi ya upandaji miti walau mitano"
Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi Allan kijazi amesema sekta Milki inamchango mkubwa katika uchumi wa Taifa lolote lile Duniani lakini kwa Tanzanis bado mchango wake ni mdogo hivyo wameitisha mkutano huo kutathimini sekta ya Ardhi na kuimarisha zaidi mchango wa sekta kiuchumi na kijamii.
Ameongeza kuwa serikali imeanzisha mchakato wa mabadiliko ya sera,sheria na maboresho kimkakati hivyo kupitia mkutano huo wadau wataweza kupata nafasi ya kutoa maoni yao juu ya mabadiliko hayo.
0 Comments