ALIYEKUWA Mtumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu ndogo Tanga Filbert Isaack Kuponewa akizungumza kuhusu kumshukuru Rais Samia Suluhu na Tanga Uwasa kwa kuwapelekea maji kwenye maeneo yao wakati wa ziara ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar iliyokuwa na lengo la kujifunza namna Tanga Uwasa ilivyotekeleza miradi ya Uviko 19 kwa ufanisi makubwa.
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa ziara hiyowa ziara ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar iliyokuwa na lengo la kujifunza namna Tanga Uwasa ilivyotekeleza miradi ya Uviko 19 kwa ufanisi makubwa.
Na Oscar Assenga,TANGA
ALIYEKUWA Mtumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu ndogo Tanga Filbert Isaack Kuponewa amemshukuru Rais Samia Suluhu na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga Uwasa kwa utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo yao na hivyo kuwaondolea kero ya muda mrefu waliokuwa nayo.
Filbert ambaye kwa sasa ni mkazi wa Kichangani Kata ya Maweni Jijini Tanga alistaafu tokea mwaka 2018, ameishukuru pia Wizara ya Maji na Tanga Uwasa kwa kuwasaidia kuwatatulia tatizo la maji ambalo lilikuwa likiwakabili kwa muda mrefu ambapo iliwalazimu kununua ndoo moja ya maji kwa sh.500.
Mstaafu huyo alisema hayo wakati wa ziara ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar iliyokuwa na lengo la kujifunza namna Tanga Uwasa ilivyotekeleza miradi ya Uviko 19 kwa ufanisi makubwa.
Wakiwa katika eneo la kichangani walitembelea wanufaika wa utekelezaji wa miradi hiyo ambapo mstaafu huyo akatoa ushuhuda huo ambapo alisema kero ya maji katika eneo hilo walikuwa nayo kwa muda mrefu ambapo ilikuwa ikiwalazimu kununua maji ndoo 500 huku akieleza mpaka amejenga nyumba yake mwaka 2010 na kumaliza alikuwa akinunua maji kupitia gari kwa sh 70,000 na likimaliza anafuata lingine.
"Ukiangalia hapa kwangu miaka ya nyuma 2010 nilikuwa nalazimika kununua ndoo ya maji kwa sh.500 kwa siku na nilikuwa natumia sh 5000 hadi 10,000 kwa siku lakin Sasa tatizo hili limekwisha kabisa namshukuru Rais Samia Suluhu,Serikali yake na Tanga Uwasa tunawaombea mwenyezi mungu awazidishie na kuwapa mafanikio Alisema Mstaafu huyo..
Awali akizungumza lengo la ziara hiyo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Maji kutoka Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar anayeshughulikia zaidi masuala ya maji Amour Abasi alisema lengo ni kujifunza namna miradi ya Uviko ilivyotekelezwa ambayo nao pia wamekuwa wakiitekeleza kwao.
Alisema kwa upande wa Tanga Uwasa miradi hiyo imeonekana kuelekea kwisha lakini wao wamekuwa wakiendelea nayo hivyo wanatumia ziara hiyo ili wapate kuona changamoto zilizokuwepo na wamepitia njia gani mpaka wao wakafanikisha miradi hiyo kwa tija kubwa.
"Tunapoona na kujifunza tutaweza kuona nasi tutatumia njia hizo kuweza kufanikisha miradi yetu maana bado hatujafikia hata asilimia 50 ya miradi hivyo ziara hii tumejifunza mengi kutokana na uwasilishwaji jinsi gani ya uharaka ulivyotumika na hivyo kufanikisha kukamilisha kwa wakati ikiwemo mambo ya tenda na mengineyo"Alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango Sera na Utafiti kutoka Wizara ya Maji,Nishati na Madini wa SMZ Dkt Mariam Issa Juma alisema wapo Tanga kwa ajili ya ziara maalumu ya kuangalia miradi ya Uviko 19 ambayo inaendelea ambapo wenzao wana uzoefu mkubwa kwa kuwa wamewatangulia na kupitia ziara hiyo utakuwa chachu ya kwenda kutekeleza vema.
Aidha alisema kwamba wameweza kuona namna ya kwenda kufanya ili kuweza kutekeleza miradi yao kwa tija na ufanisi ili kuhakikisha huduma hiyo muhimu kwa wananchi wenye uhitaji.
"Niwashukuru Wizara ya Maji ambao ndio walikubali ombi la kutupatia ziara hii ya mafunzo ningependa mashirikiano haya yaweze kuendelea katika kudumisha muungano wetu w Tanzania na Zanzibar lakini niwapongeze Tanga Uwasa kwa utekelezaji wa maji kwa ufanisi hivyo kupitia ushirikiano huu utakuwa chachu ya sisi kuweza kuona namna Bora ya uendelezaji miradi"Alisema
Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulika na Sera kutoka Wizara ya Maji nchini Teddy Mwaijumba aliwashukuru Tanga Uwasa kwa kukubali wenzao kutoka Visiwani Zanzibar kufika kwao kujifunza na kuangalia changamoto na kushauri namna ya kuzitatua huku akieleza ziara hiyo ni muendelezo wa makubaliano kati ya Wizara ya Maji Tanzania na Zanzibar kwamba wawe na mashirikiano na walisaini makubaliano.
Alisema katika makubaliano hayo kwamba wanatekeleza jambo hilo lakini hayakutoka hivihivi bali ni maelezo ya Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye ndio yenye mpango wa kuhakikisha muungano huo unaimarika kwa hiyo sekta hizo ambazo sio za muungano zinaingia makubaliano na kuna kuwa na ziara mbalimbali za mashirikiano lengo kwamba wasimuache mtu nyuma,mafanikio ya huku yaweze kuwa chachu ya wengine kujifunza ili waweze kwenda pamoja.
Akieleza namna wanavyoishukuru Serikali kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya Maji mkoani humo,Mkurugenzi Usambazaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Rashid Shabani alisema wanaishukuru Serikali kwa kuwezesha mamlaka hiyo kutekeleza miradi ya uboreshaji wa maji na uondoshwaji wa maji taka na hivi karibuni wamepatiwa fedha kutekeleza miradi mbalimbali mwaka wa fedha 2021/2022 kuelekea 2022/2023 .
Alisema katika kipindi hicho wamepokea bilioni 14 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 14 ambayo inalenga kuboresha huduma ya maji safi na uondoshaji wa maji taka katika Jiji la Tanga,Muheza na Pangani na mradi wa maji Kilindi mjini Songe.
Alisema kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa,mapambano dhidi ya UVIKo 19 Tanga Uwasa ilipokea Milioni 555,721,250 kwa ajili ya kuendeleza mtandao wa mabomba ili kufikisha karibu huduma ya maji kwa wananchi.
Alisema utekelezaji wa mradi Novemba 2021 hadi MEI 17 2022 ambapo kazi hizo I ulazaji wa mabomba jumps ha mita 17,640 katika maeneo ya kichangani-MSD mita 4000,kichangani Mji Mwema mita 5,125,Mwahako-Neema mita 3,000,Masiwani -Mbugani mita 3,300 na Pongwe-Kusini mita 2,215.
Hata hivyo alisema mradi huo umekusudi kuwahudumia watu wapatao 7,200 na mradi ulifanywa na wazabuni kwa gharama za Sh milion 512,832,602 kusimamiwa na wataalamu wa ndani na hadi swa wateja 87 wmeunganishwa kwenye mtandao wa mabomba hivyo kusaidia wakazi wapatao 522.I
0 Comments