***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imefuzu hatua inayofuata klabu bingwa Afrika baada ya kufanikiwa kuwachapa jumla ya mabao 9-0 timu ya Zalan Fc ya nchini Sudan ya Kusini.
Mechi ya kwanza Yanga ilifanikiwa kuwachapa mabao 4-0, wakati mechi ya pilia mabyo imepigwa leo katika dimba la Benjamini Mkapa imeilaza kwa mabao matano na kufanya jumla ya kuwa na mabao 9-0.
Ni Fiston Kalala Mayele amefanikiwa kufunga mabao matatu tena yaani Hat Trick baada ya mechi ya kwanza kufanya hivyo.
Mabao mengine ya Yanga yamewekwa kimyani na Farid Mussa na Aziz Ki .
0 Comments