Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba katikati, kushoto msimamizi wa Kikosi cha Mgambo 835 KJ, Kabuku jkt, Kanali Raymond Mwanri na mkuu wa jeshi la jkt nchini Meja Jenerali Rajab Mabele wakifuatilia gwaride la wahitimu.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba akikagua gwaride la wahitimu
**********************
Na Hamida Kamchalla, HANDENI.
WAHITIMU wa mafunzo ya awali ya kijeshi kwa mujibu, operesheni Jenerali Venance Mabeyo wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupelekea huduma za miundombinu ya maji na barabara katika kikosi cha 835 KJ, Mgambo jkt kilichopo Kabuku wilayani Handeni.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, Efriem Kaimu juzi wakati wakifunga mafunzo yao waliyofanya kwa muda wa miezi mitatu, alisema kwa kipindi chote walichokaa kambini hapo walikuwa na tatizo la upatikanaji wa maji.
"Katika kipindi chote cha mafunzo yetu, tumekumnana na matatizo mbalimbali, ikiwemo uhaba wa maji, tumekuwa tukipata mgao wa maji kutoka katika mradi wa maji safi na usafi wa Mazingira wa HTM, Wilaya ya Korogwe ambayo pia hayatoshelezi, hivyo hayakidhi mahitaji yetu hapa kikosini, takribani miezi mitatu sasa hatujaletewa huduma hiyo ikizingatiwa idadi kubwa ya wanafunzi" alisema.
"Hata hivyo kuna ukosefu wa miundombinu, kikosi kinahitaji kufanyiwa marekebisho katika baadhi ya barabara ambazo zinapitika kusaidia kusafirishwa mazao tunayolima pamoja na sisi wenyewe kupita wakati wote wa mafunzo, lakini pia tunaomba kikosi kuchimbwe kisima kitakachosaidia kupatikana kwa maji ya uhakika ili kuondoka kero hii" aliongeza.
Aidha Kaimu alifafanya kwamba katika mafunzo yao wamejikita katika mkakati wa jeshi hilo wa kujilisha na kujitosheleza kwa chakula ifikapo mwaka 2024/ 2025, kwa kushiriki kupalilia na kuvuna mahindi katika shamba la kimkakati la kikosi hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo aliwahakikishia wahitimu hao kuwa miundombinu hiyo Iko njiani kuboresha kwakuwa tayari serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji kuanzia kwenye mitambo ya umeme ya kudukumia maji.
"Tatizo hili Mh. Rais ameshalitambua na ameshatuwezesha kiasi cha sh milioni 200 kuanza kuondoka tope lote katika mambo wetu wa Hale, lakini pia kuhakikisha katika grid ya Taifa kunafanyika maboresho makubwa na kuhakikisha maji yanapatikana na uhakika na kwa wingi" alisema.
Mgumba alibabainisha kwamba mradi wa maji wa HTM na RUWASA wanafanya kazi zao kuhakikisha maji yanapatikana, hivyo kitendo cha kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika kikosi, siyo kosa lao bali ni tatizo la umeme.
"Haya maji tunayavuta kwa umeme, yanapita Hale na maeneo mengine, kule Hale na Pangani ambako ndiyo kuna vituo vyetu vya kupozea umeme maji yalipungua sana na kukauka kutokana na ukame, kwahiyo umeme ulikuwa unashindwa kusukuma maji yafike huku" alifafanya.
Mbali na hayo pia aliwataka wahitimu hao kwenda kuyatumia vizuri mafunzo waliyopata kuanzia kwenye ujenzi wa Taifa hadi stadi za kazi na kuepuka vitendo vibaya kwa wale watakaobahatika kuchaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali baada ya kuhitimu elimu yao ya kidato cha sita.
"Imani yangu, mnapotoka hapa na kwenda huko mwendako, mtaitumia elimu hii mliyojifunza hapa kwa vitendo, tunafahamu mliomaliza kidato cha sita ni wengi lakini siyo wote mliochaguliwa kuja hapa, mkawe walimu na mabalozi wazuri kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuja hapa" alisema.
Naye mkuu wa jeshi la kujenga Taifa (jkt), Meja Jenerali Rajab Mabele alisema lengo la mafunzo kwa vijana hao ni kukuza moyo wa uzalendo, nidhamu, ukakamavu, na nidhamu ili wajione ni sehemu ya jamii ya Watanzania, wwnaopaswa kuilinda, kuijenga, kuitetea na kuiprnda nchi yao.
"Uwepo wa mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa mawazo ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika uanzisheaji wa jeshi hili yanadumishwa, jkt maana yake ni Taifa kudai huduma ya vijana, na vijana kuitikia mwito wa kulihudumia Taifa kwa kazi yoyote inayohitajika, hivyo kauli hii inapaswa kutekelezwa kwa vitendo" alisema.
0 Comments